Thursday, January 16, 2014

FLETCHER: ‘HATUNA MCHECHETO NA CHELSEA!’


DARREN_FLETCHER-16JAN14 ANDERSON















 KIUNGO wa Manchester United, Darren Fletcher, amesema Timu yao hainachochote cha kuogopa kwa tripu ya Jumapili huko Stamford Bridge kuivaa Chelsea kwenye Mechi ya Ligi Kuu England
.
 Man United watatua Stamford Bridge wakiwa wametoka kwenye vichapo vitatu mfululizo tangu Mwaka mpya uanze na kisha kuichapa Swansea City Uwanjani Old Trafford katika Mechi yao ya mwisho ya Ligi.
Tofauti na wao, Chelsea wanapaa katika mbio za Ubingwa Msimu huu wakiwa wamekusanya Pointi 25 kati ya 30 katika Mechi zao 10 za mwisho za Ligi.
Muhimu zaidi kwa Chelsea ni ile Rekodi ya Jose Mourinho ya kutofungwa Uwanjani Stamford Bridge kwenye Ligi katika himaya zake zote mbili akiwa na Chelsea, ile ya Mwaka 2004 hadi 2007, na hii ya mara ya Pili.
Hata hivyo, Darren Fletcher, baada kurudi kwa kishindo Uwanjani kufuatia kupona kwake ugonjwa wa Tumbo uliomweka nje Mwaka mzima, amesisitiza Timu yao haina mchecheto na Mechi hiyo.
Ametamka: “Hapana, hata kidogo, sisi tunatarajiwa kushinda kila Mechi na haijali ni Swansea Nyumbani au Chelsea Ugenini. Ni maafa tusiposhinda!”
WAKATI HUO HUO, zipo taarifa kuwa Kiungo wa Man United kutoka Brazil, Anderson, yupo njiani kwenda Italy kupimwa afya na Klabu ya Fiorentina ili kuhamia huko ingawa pia inadaiwa ni kwa Mkopo.
Anderson amedumu Old Trafford kwa Miaka 6 na Nusu na kucheza karibu Mechi 100 za Ligi.
Kuondoka huku kwa Anderson ni dalili kuwa David Moyes anakaribia kumsaini Kiungo mwingine ingawa hamna uthibitisho wowote.
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
[Saa za Bongo]
Jumamosi Januari 18
1545 Sunderland v Southampton
1800 Arsenal v Fulham
1800 Crystal Palace v Stoke
1800 Man City v Cardiff
1800 Norwich v Hull
1800 West Ham v Newcastle
2030 Liverpool v Aston Villa
Jumapili Januari 19
1630 Swansea v Tottenham
1900 Chelsea v Man United
Jumatatu Januari 20
2300 West Brom v Everton
Jumanne Januari 28
2245 Man Utd v Cardiff
2245 Norwich v Newcastle
2245 Southampton v Arsenal
2245 Swansea v Fulham
2300 Crystal Palace v Hull
2300 Liverpool v Everton
Jumatano Januari 29
2245 Aston Villa v West Brom
2245 Chelsea v West Ham
2245 Sunderland v Stoke

0 comments:

Post a Comment