Sababu kubwa zinazoelezwa kuchangia hali hiyo ni
mwendelezo wa mila potofu, ndoa za jinsia moja, kurithi wajane, ndoa za
wake wengi, ukeketaji, kuachana wanandoa na umaskini wa kipato.
Akisoma risala Siku ya Ukimwi Duniani, Mwalimu
Mkuu Shule ya Msingi Nyakarima, Juma Wilson alisema takwimu za 2010-2011
zinaonyesha kuwa wanawake 261 walikutwa na maambukizi ya Virusi vya
Ukimwi, wakati wanaume walikuwa 170.
Mwaka 2011-2012, wanawake 251 waligundulika na
virusi, wakati wanaume walikuwa 133. mwaka 2012-2013 wanawake wenye
virusi walikuwa 170, wanaume 61.
Aidha, katika kampeni ya kuhamasisha watu kupima
virusi katika Wilaya ya Tarime kati ya Novemba 21 na Desemba 1,
imebainika wanawake wanaongoza kwa maambukizi. Katibu wa Afya Hospitali
ya Wilaya Tarime, Sufiani Mageta alisema katika kampeni ya kupima kwa
hiari watu 6355, kati ya hao wanawake 44 na wanaume 24 walikutwa na
maambukizi ya virusi.
Aidha akifafanua, Mageta alisema watumishi wa
Kampuni ya North Mara 1,320 waliopima kwa hiari, 30 walikutwa na
maambukizi ingawa kwa mwaka huu maambukizi yamepungua kwa asilimia 2.2
kulinganisha na mwaka jana.
Katibu Tarafa ya Inchage Machango Jonathani
aliyekuwa mgeni rasmi katika kilele cha Siku ya Ukimwi, ameitaka jamii
kuachana na mila potofu zinazochangia kuongezeka kwa maambukizi.
posted by http://thesuperonenews.blogspot.com/
posted by http://thesuperonenews.blogspot.com/
0 comments:
Post a Comment