Carlos Slim Helu.
CARLOS Slim Helu, 73, raia wa Mexico, ndiye tajiri nambari moja duniani. Utajiri wake unafikia dola bilioni 66.8 (shilingi trilioni 107). Carlos anaeleza mambo 10 ambayo yamemfanya afike hapo alipo ambayo ni haya yafuatayo;KUHUSU KAMPUNI
Muundo rahisi wa ngazi za utendaji kazi. Kubana mfumo wa uongozi, yaani kuwa na viongozi wachache. Kujali maendeleo ya wafanyakazi, kuboresha ujuzi watumishi ambao ni mhimili wa…
Carlos Slim Helu.
CARLOS Slim Helu, 73, raia wa Mexico, ndiye tajiri nambari moja duniani. Utajiri wake unafikia dola bilioni 66.8 (shilingi trilioni 107). Carlos anaeleza mambo 10 ambayo yamemfanya afike hapo alipo ambayo ni haya yafuatayo;KUHUSU KAMPUNI
Muundo rahisi wa ngazi za utendaji kazi. Kubana mfumo wa uongozi, yaani kuwa na viongozi wachache. Kujali maendeleo ya wafanyakazi, kuboresha ujuzi watumishi ambao ni mhimili wa taasisi.
UAMUZI
Utayari na uharaka wa kufanya uamuzi ni muhimu. Uendeshaji wa kampuni ndogo kwa faida ndiyo huzalisha kampuni kubwa.
MAADILI
Lazima kuzingatia maadili katika nyakati nzuri za kibiashara, badala ya kufuja ni vizuri hali hiyo iongeze uwezo, faida na maendeleo ya kampuni. Epuka kufanya uamuzi ambao unaweza kuleta matokeo magumu na ya hatari katika vipindi tata.
NI VIZURI KWENDA KISASA
Kila siku unatakiwa ujiweke katika sura mpya, ukue, ujiongezee ujuzi, ikibidi ujisomee na kupata mbinu bora za uendeshaji wa biashara kisasa. Hakikisha unazingatia ubora na ukuzaji wa bidhaa ili ziwe katika hali ya ushindani. Punguza gharama na matumizi kulingana na ulimwengu unavyokwenda.
KAMPUNI HAIPASWI KUWA NA KIKOMO
Kampuni haitakiwi kuwekewa mipaka kulingana na ukomo wa mmiliki au utawala. Mmiliki hatakiwi kuwa samaki mkubwa katika bwawa dogo, badala yake kampuni inatakiwa iwe kubwa kuliko mmiliki na utawala. Uwekezaji unatakiwa uwe mdogo katika vitu ambavyo havizalishi.
CHANGAMOTO
Hakuna changamoto ambayo inaweza kuiyumbisha kampuni kama watu wake hawatafanya kazi pamoja kwa ushirikiano. Lazima kila memba wa kampuni ajue malengo na silaha za kufanikiwa.
FAIDA PIA IWEKEZWE
Faida inapopatikana lazima iwekezwe kwa ajili ya matokeo makubwa zaidi. Fedha siku zote ndiyo huifanya kampuni ipambe moto.
UBUNIFU WENYE USHIRIKA
Ubunifu wenye ushirika katika kampuni siyo tu kwamba unakubalika kwenye biashara bali pia ndiyo suluhu ya matatizo mengi katika nchi zetu.
USTAHIMILIVU
Uimara katika utendaji na ustahimilivu wenye kusudio la kupata siku zote hutoa matokeo chanya.
MUDA
Muda wowote ni mzuri kwa watu ambao wanaweza kufanya kazi, kwa hiyo kila mmoja anatakiwa kushika muongozo huo. Posted by http://thesuperonenews.blogspot.com/
0 comments:
Post a Comment