Arsene Wenger amekiri hatastushwa ikiwa Sir Alex Fergusonatabadilika na kurudi tena kwenye Soka ndani ya Miezi 6 tangu astaafu Umeneja Manchester United.
>>PELLEGRINI: ‘SIMJUI YEYE! ALIFANYA KAZI SPAIN NA MIMI NILIKUWA KLABU NYINGINE!’
WAKATI Arsene Wenger akisema hatashangaa
ikiwa Sir Alex Ferguson atarudi tena kuongoza kwenye Soka, Manuel
Pellegrini amekataa kujitumbukiza kwenye kupigana vijembe na Jose
Mourinho huku Timu zao, Chelsea na Manchester City, zikitarajiwa kucheza
Jumapili kwenye Mechi ya Ligi Kuu England.
SOMA ZAIDI:
WENGER: ‘SIR ALEX FERGUSON ANAWEZA KURUDI!’
Ingawa Sir Alex Ferguson amesisitiza
hatarudi tena kufundisha Soka lakini Arsene Wenger, Meneja wa Arsenal,
ana wasiwasi na ametamka: “Baada Miezi 6 tutajua wazi kuhusu hili.
Huwezi kuondoka moja kwa moja. Ni kama kutumia Dawa kwa Miaka 30 na
ghafla kuacha!”
Maneno hayo ya Wenger yamekuja kwenye
Wiki ambayo Sir Alex Ferguson amezindua Kitabu chake, ‘Sir Alex
Ferguson-My Autobiography’, ambacho ndani yake ipo Sura nzima, iitwayo
‘Kushindana na Wenger’.
Akikiri kuwa hajasoma Kitabu hicho,
Wenger amesema: “Inaelekea Ferguson alikuwa akitayarisha Kitabu chake
wakati bado ni Meneja. Nadhani kila Usiku alikuwa akikaa na kuandika!”
PELLEGRINI AMDHARAU ‘MBWABWAJAJI’ MOURINHO!
Meneja wa Manchester City Manuel Pellegrini amegomakuburuzwa
na Meneja wa Chelsea Jose Mourinho na kuingizwa kwenye malumbano wakati
Timu zao zikijitayarisha kupambana kwenye Mechi ya Ligi Kuu England
huko Stamford Bridge hapo Jumapili.
Pellegrini na Mourinho wanayo historia
yao tangu huko Spain ambapo Mourinho alimbadili Pellegrini kuwa Meneja
wa Real Madrid baada ya Pellegrini kumaliza Msimu akiwa Nafasi ya Pili
nyuma ya Barcelona.
Na Mourinho amebatuka: “Nafasi ya Pili
ni Timu ya Kwanza kufungwa. Kama Real wangenifukuza mimi, nisingekwenda
Malaga! Ningekwenda kwenye Timu kubwa huko Italy au England!”
Lakini, licha ya kupigwa kijembe,
Pellegrini amekataa kuburuzwa kwenye malumbano wakati akijitayarisha
kukutana uso kwa uso na Mourinho kwa mara ya kwanza Nchini England.
Pellegrini amesema: “Huwa sijiingizi kwenye malumbano na stajiingiza sasa!”
Aliongeza: “Simjui yeye. Alifanya kazi
Spain, na mimi nilikuwa Klabu nyingine. Tulicheza Real na Malaga. Hamna
la zaidi, sina malalamiko na yeye!”
BPL: LIGI KUU ENGLAND
RATIBA
[Saa za Bongo]
Jumamosi Oktoba 26
1445 Crystal Palace v Arsenal
1700 Aston Villa v Everton
1700 Liverpool v West Brom
1700 Man United v Stoke
1700 Norwich v Cardiff
1930 Southampton v Fulham
Jumapili Oktoba 27
1630 Sunderland v Newcastle
1900 Chelsea v Man City
1900 Swansea v West Ham
1900 Tottenham v Hull
**KUANZIA JUMAPILI, MAJIRA HUKO ENGLAND YANABADILIKA.
-MECHI ZITAANZA KUCHEZWA SAA 1 MBELE YA TILIVYOZOEA BONGO
-TOFAUTI YA MASAA ITAKUWA NI MATATU [BONGO WATAKUWA SAA 3 MBELE]
0 comments:
Post a Comment