NI EL CLASICO ya 167 ndani ya Nou Camp Jijini Barcelona wakati FC Barcelona na Real Madrid zitakapocheza
Mechi ya La Liga huku macho ya Washabiki safari hii yakiwakodolea
‘Wapya’ Gareth Bale na Neymar pamoja na kuwakazia wale wale wa zamani
Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.
>>JUMAMOSI OKTOBA 26, NOU CAMP, SAA 1 USIKU
MSIMAMO-Timu za Juu:
NA |
TIMU |
P |
W |
D |
L |
F |
A |
GD |
PTS |
1 |
FC Barcelona |
9 |
8 |
1 |
0 |
28 |
6 |
22 |
25 |
2 |
Atletico de Madrid |
9 |
8 |
0 |
1 |
21 |
7 |
14 |
24 |
3 |
Real Madrid CF |
9 |
7 |
1 |
1 |
19 |
9 |
10 |
22 |
4 |
Villarreal CF |
9 |
5 |
2 |
2 |
15 |
9 |
6 |
17 |
5 |
Getafe CF |
9 |
5 |
1 |
3 |
14 |
11 |
3 |
16 |
6 |
Athletic de Bilbao |
9 |
5 |
1 |
3 |
15 |
13 |
2 |
16 |
7 |
RCD Espanyol |
9 |
4 |
2 |
3 |
12 |
11 |
1 |
14 |
Wikiendi iliyopita, Barcelona walipoteza
Pointi zao za kwanza kwenye La Liga baada ya kutoka Sare 0-0 na Osasuna
na Real Madrid kushinda na kuwakaribia Barcelona ambao wako kileleni
Pointi 3 mbele yao.
REKODI:
Uso kwa Uso:
-Real Madrid Wameshinda Mechi 90
-Barcelona Wameshinda Mechi 86
Mataji:
-Barcelona Vikombe 81
-Real Madrid Vikombe 76
Mvuto kwa El Clasico hii ni Klabu zote
mbili kuwa na Wachezaji wapya ambao wanaweza kucheza kwa mara ya kwanza
kwenye mtanange wa aina hii kwa Barcelona kumchezesha Mchezaji mpya
Neymar waliemnunua Msimu huu kutoka Santos ya Brazil na Real kumtumia
Gareth Bale alievunja Dau la kununuliwa kwa Bei Ghali Duniani
walipomnunua kwa Euro Milioni 100 kutoka Tottenham.
Lakini wakati Neymar akionyesha cheche
zake kwenye Timu ya Barcelona, Bale amekuwa akikumbwa na Majeruhi
yaliyomfanya acheze Mechi chache tu.
LA LIGA-WAFUNGAJI BORA:
1 Diego Costa [Atletico Madrid] 10
1 Lionel Messi [Barcelona] 8
3 Cristiano Ronaldo [Real Madrid] 8
4 Pedro [Barcelona] 5
Kocha wa Real, Carlo Ancelotti,
amedokeza kuwa Bale ataanza Mechi hii pamoja na Wachezaji wake wapya
wengine Isco na Asier Illarramendi huku Cristiano Ronaldo akiongoa
majeshi.
Nae, Gerardo Martino, amedokeza kuwa
mashambulizi ya Kikosi chake yataongozwa na Lionel Messi na Neymar huku
ukiwepo uwezekano wa Beki wao Mkongwe ambae pia ni Nahodha wao, Carles
Puyol, kuanza Mechi hii baada ya kurudi tena dimbani akiwa nje
akijiuguza Goti lake tangu Mwezi Machi.
MECHI ZA MWISHO:
02-03-2013 Real Madrid: 2 FC Barcelona: 1 [La Liga]
26-02-2013 FC Barcelona: 1 Real Madrid: 3 [Copa Del Rey]
30-01-2013 Real Madrid: 1 FC Barcelona: 1 [Copa Del Rey]
07-10-2012 FC Barcelona: 2 Real Madrid: 2 [La Liga]
29-08-2012 Real Madrid 2 FC Barcelona 1 [Super Cup]
23-08-2012 FC Barcelona 3 Real Madrid 2 [Super Cup]Posted by http://thesuperonenews.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment