Saturday, October 26, 2013

Sheddy Clever: Prodyuza wa ‘Number One’ aliye vichochoroni

Shadrack Willced Mongi maarufu ‘Sheddy Clever’ ndiye prodyuza wa studio hii iliyotengeneza wimbo wa ‘My Number One’ unaomilikiwa na mwanamuziki Naseeb Abdul ‘Diamond’, wimbo uliofanya vizuri katika levo za kimataifa. 

Ukiingia ndani ya studio ya Burn Records iliyopo Tabata, jijini Dar es Salaam, huwezi kuamini kama ndiyo sehemu ‘zinakopikwa’ kazi za baadhi ya wasanii zinazowafanya kuwa maarufu na kuwaingizia kipato, kupitia shoo na mialiko ya ndani na nje ya nchi.
Studio hii iliyopo maeneo ya ‘uswahili’ imezingirwa na nyumba nyingi kiasi cha kushindwa kuijua njia kwa uharaka zaidi pale mtu anapotaka kufika kwa prodyuza huyo. Studio hii ni ndogo yenye vifaa vichache tu vya kimuziki lakini yenye prodyuza makini na mwenye kipaji.
Shadrack Willced Mongi maarufu ‘Sheddy Clever’ ndiye prodyuza wa studio hii iliyotengeneza wimbo wa ‘My Number One’ unaomilikiwa na mwanamuziki Naseeb Abdul ‘Diamond’, wimbo uliofanya vizuri katika levo za kimataifa.
Hata hivyo sehemu ya mahojiano na mwandishi wa Starehe ni kama ifuatavyo;
Swali: Mbona Studio yako ipo uchochoroni hivi?
Jibu: Unasema uchochoroni!  Wasanii wengi wamekuja hapa na wanatumia muda mwingi kuwepo ndani ya studio hii huku wakitumia vyakula vya hukuhuku kwetu uswahili, si jambo la ajabu. Lakini ni mazoea tu kwetu tunaona sawa na kwa upande wangu inanipa hamasa kwani najisikia huru kufanya kazi nikiwa maeneo haya.
Swali: Ndiyo kusema Diamond alikuja kurekodi kwenye studio hii?
Jibu: Ndiyo alikuja kurekodi katika studio hii na alikuwa akikaa hapa kutwa nzima. Yule jamaa anafanya kazi sijawahi ona kutoka kwa wasanii wengine akija hapa anatumia muda mwingi kujenga mashairi, hata hivyo anatumia akili kubwa sana katika kufanya kazi si sawa na vile watu wanamwona. Korasi ya wimbo wa My Number One tulitumia zaidi ya saa 12 kuitengeneza na saa nyingine 12 kuirekebisha, yupo makini sana. Ilichukua miezi sita kukamilika.
Swali: Ilikuwaje akapajua hapa?
Jibu: Diamond alinitafuta yeye mwenyewe, ilikuwa saa mbili asubuhi akanipigia na kunifahamisha jina lake akasema anakuja, kwa kuwa namba niliyokuwa nayo alishaacha kuitumia nilidhani si yeye lakini baada ya muda nikashangaa amefika. Alinitaka nimsikilizishe midundo nami nilifanya hivyo hatimaye akapenda mmoja wapo, basi tulipeana mikakati kazi ikafanyika.
Swali: Kazi uliyoifanya imeweza kumwingizia kitita kikubwa cha pesa mwanamuziki huyo vipi kwa upande wako inakuneemesha vipi?
Jibu: Hapana nilimfanyia kazi akanilipa ujira wangu mzuri tu, hivyo huko mbele ni kazi yake. Lakini katika upande wa hatimiliki hivi sasa tupo mbioni kuhakikisha chama chetu cha maprodyuza  cha Tanzania TSPA kinasajiliwa ili kuweza kutetea kazi zetu na hatimiliki posted byhttp://thesuperonenews.blogspot.com.

0 comments:

Post a Comment