LIGI KUU ENGLAND ipo dimbani Jumamosi na Jumapili kabla kuwa nje kwa Wiki mbili kupishaMechi za Kimataifa.
STADIUM OF LIGHT: SUNDERLAND v MAN UNITED!
VINARA ARSENAL, CHELSEA UGENINI JUMAPILI, SPURS NYUMBANI!
IFUATAYO NI TAARIFA/RATIBA YA MECHI ZA WIKIENDI:
RATIBA:
BPL: LIGI KUU ENGLAND
[Saa za Bongo]
Jumamosi 5 Oktoba
14:45 Manchester City v Everton
17:00 Cardiff City v Newcastle United
17:00 Fulham v Stoke City
17:00 Hull City v Aston Villa
17:00 Liverpool v Crystal Palace
19:30 Sunderland v Manchester United
Jumapili 6 Oktoba
15:30 Norwich City v Chelsea
15:30 Southampton v Swansea City
18:00 West Bromwich Albion v Arsenal
18:00 Tottenham Hotspur v West Ham United
SUNDERLAND V MANCHESTER UNITED
-Stadium of Light
Hii ni Mechi inayokodolewa macho na
wengi huku wengine wakinoa visu kutaka kumnanga Meneja David Moyes wa
Manchester United kwa madai ya Mabingwa hao kuanza vibaya Msimu huu.
Ni kweli, baada ya kufungwa 2-1 na West Bromwich Albion Wikiendi iliyopita, kumezidisha presha kwa Moyes na Man United.
Lakini, baada ya kucheza vizuri Ugenini
huko Ukraine walipotoka Sare na Shakhtar Donetsk ambako, katika Mechi 5
hakuna Timu ya England hata moja, hasa Chelsea na Arsenal, zilizotoka
bila kipigo, Jumamosi Man United wanaelekea huko Stadium of Light kwa
Sunderland, Timu isiyo na Meneja baada kutimuliwa Paolo Di Canio, na
ndio Timu ambayo haina Pointi hata moja kwa Mechi za Nyumbani na pia
ndio Timu pekee haijashinda kwenye Ligi Msimu huu.
MANCHESTER CITY V EVERTON
-Etihad Stadium
Everton, ambao ndio Timu pekee
haijafungwa kwenye Ligi Msimu huu, wanasafiri kwenda kukutana na Man
City ambayo Juzi ilibandikwa Bao 3-1 hapo hapo kwao na Mabingwa wa Ulaya
Bayern Munich kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Kipigo hicho kilifuata kile Wikiendi iliyopita walipochapwa 3-2 na Aston Villa kwenye Ligi.
Uwanjani Etihad, Everton wamefungwa na City Mechi moja tu kati ya 6 walizocheza mwisho.
Everton ya sasa, chini ya Meneja mpya Roberto Mancini, inamtumia Kijana mdogo Ross Barkley ambae ameonyesha uwezo mkubwa.
Je Manuel Pellegrin, Meneja mpya wa Man City, ataiinua Timu yake toka kipigo cha Wikiendi iliyopita na Juzi?
CARDIFF CITY V NEWCASTLE UNITED
-Cardiff City Stadium
Mara ya mwisho kukutana Mwaka 2010
Newcastle iliibamizi Cardiff Bao 5 katika Ligi Daraja la Championship
lakini Cardiff ya Ligi Kuu iko ngumu na Wikiendi iliyopita walishinda
Ugenini walipoifunga Fulham kwa Bao la masafa marefu la Jordan Mutch.
Newcastle, kwa sasa, wana mtambo wa Magoli Loic Remy ambae amefunga Bao 3 katika Mechi 4 zilizopita.
FULHAM V STOKE CITY
-Craven Cottage
Stoke hawajashinda kwenye Ligi tangu Agosti na mara ya mwisho dhidi ya Norwich walicheza ovyo.
Lakini huu ni wakati muafaka kukutana na
Fulham ambao wana Pointi moja tu katika Mechi zao 7 za Nyumbani huku
Staa wao Dimitar Berbatov akiwa hana Goli la Ligi Msimu huu na Mashabiki
washaanza kuweka Mabango Meneja Martin Jol aondolewe.
HULL CITY V ASTON VILLA
-KC Stadium
Hull City, Timu iliyopanda Daraja Msimu
huu na ipo chini ya Mchezaji wa zamani wa Manchester United, Steve
Bruce, haijafungwa katika Mechi 3.
Lakini Aston Villa ni Timu iliyokuja juu
sasa na Wikiendi iliyopita iliichapa Man City Bao 3-2 na tena walicheza
bila Mastraika wao wa kutumainiwa Christian Benteke na Gabriel
Agbonlaho.
Tatizo kubwa la Aston Villa ni Difensi yao inayovuja na Wikiendi iliyopita walifungwa Bao lao la 1,000 kwenye Ligi Kuu.
LIVERPOOL V CRYSTAL PALACE
-Anfield
Crystal Palace wako Nafasi ya Pili toka Mkiani na Meneja wao, Ian Holloway, ameitaka Timu yake ikaze Buti.
Lakini huko Anfield kibarua wanacho cha kupambana na Mastraika hatari wa Liverpool, Daniel Sturridge na Luis Suarez.
NORWICH CITY V CHELSEA
-Carrow Road
Kila Timu Wikiendi iliyopita ilifuta
kikwazo cha kutofunga Magoli kwa Norwich kumaliza Dakika 235 za Mechi za
Ligi bila kufunga kwa Goli la Jonny Howson walipoifunga Stoke na Kichwa
cha John Terry kilimaliza Dakika 247 za Chelsea kutofunga Bao Ugenini
kwenye Ligi.
SOUTHAMPTON V SWANSEA CITY
-St Mary’s Stadium
Msimu huu Swansea wameshacheza na Timu 3
za juu, pamoja na Manchester United, katika Mechi zao 6 za kwanza na
matokeo mazuri katika Mechi hizo ni Sare na Liverpool.
Swansea wanatarajia kuimarika kwenye
Difensi kufuatia kurudi baada kupona kwa Sentahafu wao Ashley Williams
na hivyo kuwa imara ziadi ya ile Mechi na Arsenal waliyoruhusu Bao 2
katika Dakika 4.
Southampton walipata ushindi wao wa
kwanza wa Nyumbani wakati Straika wao wa England, Rickie Lambert,
alipofunga kwa frikiki safi dhidi ya Crystal Palace.
TOTTENHAN HOTSPUR V WEST HAM UNITED
-White Hart Lane
West Ham wamecheza Ugenini mara 3 Msimu
huu na kuambua Pointi 2 bila Goli na hii si rekodi murua ya kuingia nayo
White Hart Lane kucheza na Tottenham ambayo inafunga Magoli kirahisi
kupitia Mastraika wao Jermaine Defoe, Roberto Soldado na sasa Gylfi
Sigurdsson ambae amefunga Bao 3 katika Mechi 5 zilizopita.
WEST BROMWICH ALBION V ARSENAL
-The Hawthorns
Arsenal, Vinara wa Ligi, wanasaka rekodi
ya ushindi wao wa 9 mfululizo Ugenini lakini wanatua The Hawthorns,
Nyumbani kwa WBA, ambayo Wikiendi iliyopita waliifunga Man United 2-1
huko Old Trafford.
Mwezi uliopita, Uwanjani hapa kwenye Capital One Cup, WBA na Arsenal zilitoka 1-1 na Arsenal kusonga kwa Penati 4-3.
MSIMAMO:
NA | TIMU | P | GD | PTS |
1 | Arsenal | 6 | 6 | 15 |
2 | Liverpool | 6 | 4 | 13 |
3 | Tottenham | 6 | 4 | 13 |
4 | Everton | 6 | 3 | 12 |
5 | Chelsea | 6 | 4 | 11 |
6 | Southampton | 6 | 3 | 11 |
7 | Man City | 6 | 7 | 10 |
8 | Hull | 6 | -1 | 10 |
9 | Aston Villa | 6 | 1 | 9 |
10 | West Brom | 6 | 1 | 8 |
11 | Cardiff | 6 | -1 | 8 |
12 | Man Utd | 6 | 0 | 7 |
13 | Swansea | 6 | -1 | 7 |
14 | Norwich | 6 | -2 | 7 |
15 | Stoke | 6 | -2 | 7 |
16 | Newcastle | 6 | -4 | 7 |
17 | West Ham | 6 | -1 | 5 |
18 | Fulham | 6 | -5 | 4 |
19 | Crystal Palace | 6 | -6 | 3 |
20 | Sunderland | 6 | -10 | 1 |
MECHI ZIJAZO:
Jumamosi 19 Oktoba
14:45 Newcastle United v Liverpool
17:00 Arsenal v Norwich City
17:00 Chelsea v Cardiff City
17:00 Everton v Hull City
17:00 Manchester United v Southampton
17:00 Stoke City v West Bromwich Albion
17:00 Swansea City vSunderland
19:30 West Ham United v Manchester City
Jumapili 20 Oktoba
18:00 Aston Villa v Tottenham Hotspur
Jumatatu 21 Oktoba
22:00 Crystal Palace v Fulham
0 comments:
Post a Comment