Wednesday, October 9, 2013

DIAMOND AJITABIRIA KIFO DAR




KINARA wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ametumia melodi inayofanana kwa mbali na wimbo wake wa Kesho, kutengeneza ngoma mpya inayoitwa Kama Nikifa Kesho inayozungumzia hali itakavyokuwa baada ya yeye kufa, jambo lililotafsiriwa na mashabiki wake kuwa ni uchuro wa kujitabiria kifo..........................................................

Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
Sikiliza wimbo huo wa Diamonda hapa:
Katika wimbo huo aliouachia kwenye Mtandao wa You Tube na kusambaa katika mitandao ya kijamii mwishoni mwa wiki iliyopita, Diamond aliibua gumzo kubwa kwa mashabiki wake kufuatia aina ya mashairi aliyotumia kuelezea hali itakavyokuwa baada ya kifo chake.
Sehemu ya mashairi yake yanasema:
“Vipi Maneke (prodyuza) atanililia? Je, wasanii wenzangu wataniimbia? Ama litafutika jina langu na nyimbo zangu hawatasikia? Vipi wasafi watanililia? Je, ndugu, rafiki watahudhuria? Ama nitakapokufa sina changu hata mama’angu watamkimbia?
“Ni swali gumu sana lakini ipo siku ikifika…nauliza nikifa kesho nani atamwambia mama’angu asi-cry? Sijui wengi watalia kwa uchungu au watafurahi…?
Ooh mama’angu! Mwanao sina mtoto hata mmoja hivyo nikiondoka wasikudanganye… wengi waliniambia ngojangoja, muda wao haujawadia… Wengine wakakataa tusizae… wataharibu ujana wao…waliniumiza sana.”
Baadhi ya mashabiki wake walikuwa na maoni tofauti mitandaoni.
“Steven Kanumba alifanya hivihivi. Aliimba wimbo (Nitainua Macho) ulioonesha kama alijua atapatwa na umauti.
“Pia kwenye wimbo wa Ngwea (Marehemu Albert Mangweha) alioachia siku chache kabla ya kifo wa No Beef aliomshirikisha TID kuna sehemu ya mashairi anasema: Yule Ngwea wa zamani amesha-R.I.P (ameshafariki dunia), utadhani alijua kinachofuata,” aliandika Paulkwere akitoa maoni ya wimbo huo kwenye Twitter.
“Acheni hizo, ninyi ndiyo mnamchuria kwa sababu siri ya kifo anaijua Mungu tu,” ilisomeka sehemu ya maoni katika ukurasa wa Diamond wa Facebook.
Hata hivyo, gazeti hili lilipomtafuta Diamond ili kuzungumzia ishu hiyo kiundani simu yake ya kiganjani iliita bila kupokelewa.Posted by Thesuperonenews.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment