NAHODHA Nemanja Vidic anaamini Manchester United inaweza kugombea Ubingwa wa Ligi ikiwa tu Difensi yao inayovuja itazibwa.
JUMAMOSI STADIUM OF LIGHT NA SUNDERLAND!
Man United, ambao katika Mechi yao ya
mwisho ya Ligi Kuu England walichapwa 2-1 na West Bromwich Albion
Uwanjani Old Trafford, wapo Nafasi ya 12 baada ya Mechi 6.
-TAKWIMU
-Manchester United wapo Nafasi ya 12 kwenye Ligi.
-Wamefungwa Mechi 3 kati ya 6 za Ligi walizocheza.
-Huu ni mwanzo mbovu kwa Miaka 24 tangu
Mwaka 1989/90, Sir Alex Ferguson alipoiongoza Timu na kuambua Pointi 7
katika Mechi 6 kama ilivyo sasa.
Jumamosi Man United wapo Ugenini huko
Stadium of Light kucheza na Sunderland isiyokuwa na Meneja baada
kutimuliwa Paolo Di Canio.
HIMAYA YA DAVID MOYES-MATOKEO:
-MECHI 10: Ushindi 5 Sare 2 Kufungwa 3
Oktoba 2013
2 Oktoba: Shakhtar Donetsk 1 Man United 1[UCL]
Septemba 2013
28 Septemba: Man United 1 West Brom 2 [BPL]
25 Septemba: Man United 1 Liverpool 0 [COC]
22 Septemba: Man City 4 Man United 1 [BPL]
17 Septemba: Man United 4 Bayer 04 Leverkusen 2 [UCL]
14 Septemba: Man United 2 Crystal Palace 0 [BPL]
28 Septemba: Liverpool 1 Man Utd 0 [BPL]
Agosti 2013
26 Agosti: Man Utd 0 Chelsea 0 [BPL]
17 Agosti: Swansea 1 Man Utd 4 [BPL]
11 Agosti: Man Utd 2 Wigan 0 [Ngao ya Jamii]
**UCL=UEFA CHAMPIONS LIGI
**BPL=LIGI KUU ENGLAND
**COC=CAPITAL ONE CUP
Vidic amesema: “Lazima tukubali,
hatukuanza vizuri. Hatukuwa tukipata uchezaji tunaotaka na tuwe wakweli
tukubali tumefanya makosa. Timu hii inao uwezo mkubwa na tunafanyia kazi
vizuri. Mara nyingine matokeo hayaji, mara nyingine uchezaji mzuri
haupo. Lakini matumaini yapo. Kitu muhimu ni kujihami vizuri. Tukijihami
vizuri, tuna nafasi kubwa ya kutwaa Mataji! ”
Hata hivyo yapo matumaini makubwa kuwa
mambo yatabadilika, na kama Meneja wao David Moyes alivyodokeza, tayari
washacheza na wapinzani wao wakubwa Man City, Liverpool na Arsenal na
sasa ni kutia mkazo Mechi nyingine.
Na Vidic amesema kuwa Mechi ijayo na Sunderland ndio muhimu zaidi.
Kwa Mechi hiyo na Sunderland, Wayne
Rooney, ambae aliikosa Mechi ya Jumatano na Shakhtar Donetsk baada
kuumia Mazoezini, atakuwepo.
MOYES==KIMBEMBE KINACHOMNGOJA
[Saa za Bongo]
OKTOBA |
SAA |
SIKU |
|
BPL |
Sunderland v Man United |
19:30 |
Jumamosi Oktoba 5 |
BPL |
Man United v Southampton |
17:00 |
Jumamosi Oktoba 19 |
UCL |
Man United v Real Sociedad |
21:45 |
Jumatano Oktoba 23 |
BPL |
Man United v Stoke |
17:00 |
Jumamosi Oktoba 26 |
COC |
Man United v Norwich City |
22:45 |
Jumanne Oktoba 29 |
NOVEMBA |
|||
BPL |
Fulham v Man United |
18:00 |
Jumamosi Novemba 2 |
UCL |
Real Sociedad v Man United |
22:45 |
Jumanne Novemba 5 |
BPL |
Man United v Arsenal |
19:10 |
Jumapili Novemba 10 |
BPL |
Cardiff v Man United |
19:00 |
Jumapili Novemba 24 |
UCL |
Bayer Leverkusen v Man United |
22:45 |
Jumatano Novemba 27 |
BPL=LIGI KUU ENGLAND |
|||
UCL=UEFA CHAMPIONZ LIGI |
|||
COC=CAPITAL ONE CUP |
0 comments:
Post a Comment