Mtoto
EMILLY GEORGE[7] Mkazi wa kijiji cha RUANDA wilaya ya Mbeya akilia kwa
uchungu maumivu ya vidonda baada ya kuchomwa moto na mama yake mzazi
kisa akidaiwa kuiba mayai ya kuku jamani ukatili gani huu?
Wimbi la ukatili dhidi ya watoto bado
limezidi kuchukua sura mpya baada ya mtoto EMILLY GEORGE[7] Mkazi wa
kijiji cha RUANDA wilaya ya Mbeya kuunguzwa vibaya mikono yote miwili na
mama yake mzazi ELESIA MWASILE[41] kwa maji ya moto kisha kufungiwa
ndani kwa siku saba bila matibabu yoyote.
Akiongea huku akitetemeka kwa hofu
ELESIA amesema kuwa chanzo cha cha kumchoma mtoto huyo ni kutokana na
malalamiko ya majirani wakimtuhumu mtoto huyo kujihusisha na vitendo vya
wizi vikiwemo wizi wa pesa na mayai ya kuku.
Tukio la mwisho lililopelekea mtoto
huyo hadi kuchomwa ni pale ilipodaiwa na mama huyo kuwa mtoto aliiba
mayai akidai amechoshwa na tabia za malalamiko ya mara kwa mara kutoka
kwa jirani zake.
Baada ya kuunguzwa kikatili mtoto huyo
alifungiwa ndani kwa siku saba bila matibabu yoyote hali iliyowafanya
majirani kuuliza aliko mtoto kutokana na mtoto huyo kutoonekana mitaani
hali iliyopelekea kutolewa taarifa ofisi ya kijiji ili kubaini aliko
mtoto.
Uongozi wa kijiji baada ya kupata
taarifa kwa majirani walifanya upekuzi na kumkuta mtoto amefungiwa ndani
huku akiwa na majeraha makubwa katika mikono yote miwili ndipo taarifa
ilitolewa kituo cha Polisi MBALIZI ambapo mama huyo alikamatwa.
Baada ya kukamatwa mama huyo katili
alkabidhiwa kwa Dawati la Polisi Jinsia na watoto chini ya Kiongozi wa
Wilaya D\SSGT PUDENSIANA BAITU na Mwenyekiti MARY GUMBO ambaye muda wote
alikuwa akiangua kilio kutokana na kitendo alichofanyiwa mtoto na mama
yake mzazi.
Hivi sasa mwanamke huyo anahojiwa na
Polisi kituo kikuu cha kati na atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma hizo
na mtoto amelazwa katika Hospitali ya Rufaa wadi namba tano akiendelea
kupatiwa matibabu.
Vitendo vya unyanyasaji vimendelea
kukemewa Mkoani Mbeya na Asasi mbalimbali hasa kwa watoto vikiwemo vya
ubakwaji,ulawiti,kazi za ndani na baadhi ya watoto wamepata ulemavu wa
kudumu ikiwemo kupoteza viungo.
Mama mzazi wa mtoto aliyechomwa moto ELESIA MWASILE[41] akipelekwa kituoni na wanausalama
Hapa wanausalama na mama mzazi wa mtoto huyo wakielekea kumwona mtoto huyo katika hospitali ya Rufaa MbeYA
Baada ya kukamatwa mama huyo katili alikabidhiwa kwa Dawati la Polisi Jinsia na watoto chini ya Kiongozi wa Wilaya D\SSGT PUDENSIANA BAITU akimjulia hali mtoto Emilly
Baada ya kukamatwa mama huyo katili alikabidhiwa kwa Dawati la Polisi Jinsia na watoto chini ya Kiongozi wa Wilaya D\SSGT PUDENSIANA BAITU akimjulia hali mtoto Emilly
0 comments:
Post a Comment