LEO huko Lubumbashi, Congo DR, TP Mazembe imetinga Nusu Fainali ya Mashindano ya CAF ya Kombe
la Shirikisho baada ya kuichapa Entente Sportive de Sétif ya Algeria
Bao 4-2 huku Bao mbili za Mazembe zikifungwa na Straika wa Tanzania,
Thomas Ulimwengu, na moja la mwenzake Mbwana Samatta.
KOMBE LA SHIRIKISHO
ULIMWENGU BAO 2, SAMATTA 1!!
MSIMAMO:
[Kila Timu imecheza Mechi 4 isipokuwa inapotajwa]
KUNDI A
1 Club Sportif Sfaxien Pointi 12
2 E. S. Sahel 4
3 Stade Malien de Bamako 4
4 St George SA 3
KUNDI B
1 TP Mazembe Mechi 5 Pointi 10**IMETINGA NUSU FAINALI
2 C. A. Bizertin 5
3 FUS de Rabat 5
4 ES de Setif Mechi 5 Pointi 3
Ulimwengu alipiga Bao la kwanza katika Dakika ya 4 kwa kichwa lakini Setif wakasawazisha Dakika moja baadae.
Tesor Mputu akaifungia Mazembe Bao la
Pili katika Dakika ya 16 na Dakika ya 27 Ulimwengu akapiga Bao la 3
kufuatia krosi ya Mbwana Samatta.
Katika Dakika ya 64, Mbwana Samatta akaipigia TP Mazembe Bao la 4 na Setif kufunga Bao lao la pili Dakika ya 71.
Katika Dakika ya 91, TP Mazembe walipewa Penati lakini Ngasanya Ilongo akapiga nje.
TP Mazembe wametinga Nusu Fainali huku
wakiwa na Mechi moja mkononi ambayo watamalizia Ugenini kwa kwa kucheza
na FUS Rabat ya Morocco.Posted by Thesuperonenews.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment