Wednesday, August 7, 2013

MESSI, RIBÉRY NA RONALDO NANI KUWA MCHEZAJI BORA ULAYA:

UEFA_BEST_PLAYER

Lionel Messi, Franck Ribéry na Cristiano Ronaldo ndio wameteuliwa kuwemo kwenye Listi yamwisho ya kugombea Tuzo ya UEFA ya Mchezaji Bora Ulaya kwa Msimu wa 2012/13 itakayofanyika Agosti 29 kwa kupigiwa Kura Laivu.
Wachezaji hao watatu ndio walipata Kura nyingi za Wanahabari kutoka Nchi Wanachama wa UEFA kati ya Wachezaji 10 walioteuliwa awali.
DONDOO MUHIMU:
-Hii ni Tuzo ya Tatu ya UEFA ya Mchezaji Bora wa Mwaka tangu ianzishwe kutokana na juhudi za Rais wa UEFA, Michel Platini, akishirikiana na Kundi la European Sports Media (ESM).
-Andrés Iniesta alitwaa Tuzo ya 2011/12 na  Messi kutwaa Tuzo ya kwanza kabisa ilipoanzishwa tu Msimu wa 2010/11.
Mshindi atapatikana Agosti 29 kwenye Kura za Laivu zitakazofanyika wakati wa kuendesha Droo ya Makundi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI huko Monaco.
Lionel Messi alitwaa Ubingwa wa La Liga akiwa na Barcelona Msimu uliopita na pia kutwaa Taji la FIFA Ballon d’Or ikiwa ni mara yake ya tano mfululizo huku akifunga Jumla ya Mabao 46 ya Ligi Msimu uliopita.
Franck Ribery aliiongoza Bayern Munich kutwaa ‘Trebo’ kwa kushinda Taji la UEFA CHAMPIONZ LIGI, Ubingwa wa Bundesliga na pia German Cup.
Cristiano Ronaldo alikuwa ndie Mfungaji Bora wa Msimu wa 2012/13 wa UEFA CHAMPIONZ LIGI kwa kufunga Bao 12 na pia Msimu huo huo kuvuka Magoli 100 kwa Timu ya Taifa ya Portugal.
Huko Monaco, kwenye Kura Laivu ya kumteua Mchezaji Bora, Wanahabari watatumia Mfumo wa Elektroniki.
WACHEZAJI WALIOSHIKA NAFASI ZA 4 HADI 10:
4 Robert Lewandowski (POL) – Borussia Dortmund (Pointi 80)
5 Arjen Robben (NED) – FC Bayern München (55)
6 Thomas Müller (GER) – FC Bayern München (51)
7 Gareth Bale (WAL) – Tottenham Hotspur FC (48)
8 Bastian Schweinsteiger (GER) – FC Bayern München (34)
9 Zlatan Ibrahimović (SWE) – Paris Saint-Germain FC (27)
10 Robin van Persie (NED) – Manchester United FC (24)

0 comments:

Post a Comment