Wednesday, August 7, 2013

JOSE MOURINHO LEO WATANIKOMA, REAL MADRID: LEO USIKU NA CHELSEA FAINALI HUKO USA!

RONALDO-AUG13
KOMBE: Guinness International Champions Cup
UWANJA: Sun Life, Miami Gardens, Florida, USA
MUDA: SAA 10 ALFAJIRI [Bongo Taimu] Jumatano kuamkia Alhamisi Agosti 8

Real Madrid na Chelsea zinakutana leo Usiku huko Florida, USA kwenye Fainali ya Guinness International Champions Cup kwenye Mechi yenye mvuto hasa kuhusiana na Mameneja wao.
Mwaka mmoja uliopita, Jose Mourinho alikuwa Meneja wa Real Madrid na sasa yupo Chelsea wakati Carlo Ancelotti alikuwa Chelsea na sasa yupo Real Madrid.
Timu zao zote za sasa za Mameneja hao zinaingia kwenye Mechi hii zikiwa hazijafungwa katika Mechi zao zote za majaribio kabla Msimu mpya kuanza.
Kwenye Fainali hii ya leo, Chelsea wametinga baada ya kuzifunga Klabu za Italy, Inter Milan na AC Milan, zote Bao 2-0 kila moja, na Real Madrid waliifunga LA Galaxy Bao 3-1 na Everton 2-1.
Kila Timu inaingia kwenye Mechi hii huku Wachezaji wao waking’ara katika Mechi zao za hivi karibuni na kwa Chelsea wapya wao, Marco van Ginkel, André Schürrle na Kevin De Bruyne, CARLO_ANCELOTTIwameonyesha cheche zao wakisaidiana na wa zamani kina Eden Hazard, Victor Moses, GaryMOURINHO-CHELSEA_TRAININGCahill, Branislav Ivanović na Ramires.
Nao Real Madrid,wakiwa na wachezeji wao kama akina Mesut Özil, Ángel di María, Karim Benzema, Kaká, Xabi Alonso, Sergio Ramos, Sami Khedira na Kipa Iker Casillas, wameonyesha wamekamilika kila idara.
Lakini pia Mechi hii imeongezewa chumvi hivi Juzi baada ya Jose Mourinho kubatuka kuhusu Cristiano Ronaldo na hilo kuchukuliwa kama dharau.
Mourinho, alipokuwa akihojiwa na Vyombo vya Habari vya Spain, alidai kuwa akiwa na Miaka 30 alimfundisha ‘Ronaldo wa kweli, na si huyu mwingine, ni Ronaldo Mbrazil’ akimaanisha wakati wake alipokuwa Msaidizi wa Kocha kwenye Klabu ya Barcelona.
Na Ronaldo alijibu: “Kuna vitu vingine kwenye maisha havifai hata kuvizungumzia na hili ni wazi kabisa!”
Aliongeza: “Huwa napenda kuyakumbuka mazuri ya Makocha. Sitemei mate sahani ambayo nakulia na siongelei Watu wengine wanaosema mabaya kuhusu mimi! Tutakutana na Chelsea na si Kocha wao. Ni Gemu nyingine ya kujipasha moto na tunategemea kushinda ili tuanze La Liga katika hali njema!”
VIKOSI VINATARAJIWA:
REAL MADRID: Casillas; Carvajal, Varane, Pepe, Marcelo; Alonso, Khedira; Di Maria, Ozil, Ronaldo; Benzema. l
CHELSEA: Cech; Cole, Ivanovic, Luiz, Azpilicueta; Van Ginkel, Mikel; De Bruyne, Oscar, Hazard; Lukaku
Endelea kufatatilia katika mtandao huu utapata matokeo live mpaka metch inaisha

0 comments:

Post a Comment