Mshambuliaji huyu amekuwa akihusishwa na kujiunga na klabu vya Arsenal huku ofa mbili tayari zikiwa zimekataliwa na Liverpool - ikiwemo ya £40m ambayo mshambuliaji huyo anasema ilitenguwa kifungu cha kumruhusu kuuzwa kwenye mkataba wake ambao alisaini miezi 12 iliyopita.
"Mwaka jana nilipata nafasi ya kujiunga na klabu kubwa barani ulaya lakini niliamua kubaki kwa maelewano kwamba ikiwa msimu huu ingeshindikana kufuzu kucheza Champions League basi ningeruhusiwa kuondoka," Suarez ameliambia gazeti la Guardian.
"Nilijitoa kwa yote msimu uliopita lakini haikutosha kutufanya kumaliza kwenye top 4 - sasa ninachokitaka ni Liverpool kuheshimu maelewano yetu."
Suarez pia ameonyesha wazi yupo tayari kuipeleka kesi yake kwa kamati ya Premier League ili kuhakikisha azma yake inafanikiwa.
Aliendelea: "Walinipa ahadi na tuliandika mkataba kuhusu hilo na sasa nipo tayari kulipeleka hili suala Premier League ili wao waamue kesi hii lakini sihitaji suala hili lifikie huko.
"Sidhani kama nimesalitiwa, lakini klabu iliniahidi mwaka mmoja uliopita na mimi nilifanya hivyo kwa kuwaambia kama tutafuzu ikiwa tungepata nafasi ya kushiriki Champions League.
"Walinipa ahadi hiyo mwaka mmoja uliopita na sasa nataka waheshimu ahadi yao. Sio kitu tulichokubaliana kwa mdomo tu bali kiandikwa kwenye mkataba. Siendi kwenye kwenye klabu nyingine ili kuiumiza Liverpool
Psted by Thesuperonenews.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment