Wednesday, August 7, 2013

MOYES: ROONEY, ATAKIWIKUSHAWISHIKA NA AJIPA NA KIKOSI WAPYA WATAKUJA KABLA DIRISHA KUFUNGWA!’

DAVID_MOYES-INSTRUCTING 














 BOSI wa Manchester United David Moyes amesisitiza Wachezaji wapya watatua Old Trafford kabla Dirisha la Uhamisho kufungwa.


Hadi sasa, katika Kipindi hiki cha Uhamisho, Man United imemsaini Beki Chipukizi wa Uruguay Guillermo Valera pekee na pengine huyo hatakuwemo kwenye Kikosi cha Kwanza.
Mpaka wakati huu inaaminika Man United imeshindwa kuwasaini Thiago Alcantara, Cesc Fabregas na Leighton Baines lakini Moyes, akiongea Jana Usiku baada ya Mechi ya Kirafiki huko Stockholm, Sweden waliyotoka 1-1 na AIK, amesema: “Nadhani tutaleta Wachezaji kabla Dirisha kufungwa. Tunaendelea vizuri lakini ukiniuliza tupo karibu? Siwezi kukupa jibu!”
Akaongeza: “Nipo burudani, hapa tuna Kikosi thabiti na ndio hicho hicho kilichotwaa Ubingwa. Huwezi kujua lolote hadi Msimu uanze.”
Akibanwa kuhusu sakata la Wayne Rooney kudaiwa kutaka kuhama huku Chelsea ikitoa Ofa yao ya pili kumnunua ambayo ilikataliwa, Moyes alijibu kuwa hana lazima ya kumshurutisha Mtu kubaki Old Trafford.
Alipoulizwa moja kwa moja ni nini Rooney amesema baada ya Man United kuikataa Ofa ya Pili ya Chelsea, Moyes alijibu: “Sijui, sijamuuliza hilo.”
Na alipobanwa ikiwa upo ulazima wa kumbembeleza Rooney kubaki Man United, Moyes alisema: “Huhitaji kumrubuni Mtu kuichezea Manchester United!”
Hilo ni jibu ambalo linamaanisha Wachezaji ndio wanaotaka kuichezea Klabu kubwa Man United na si Klabu kubembeleza Wachezaji.
Lakini Moyes alisisitiza kuwa nia yao ni kumfanya Rooney awe fiti ili acheze Mechi zijazo haraka iwezekanavyo.
Alisema: “Alirudi toka mapumziko akiwa safi lakini alipata maumivu kadhaa na sasa hajacheza Mechi na hilo tunalifikiria.”
Alipoulizwa kama Rooney atacheza Jumapili huko Wembley kwenye Mechi na Wigan kugombea Ngao ya Jamii, Moyes alijibu: “Sina tatizo yeye kucheza lakini hatakuwa fiti. Ipo nafasi anaweza kucheza lakini nafikiri hatakuwa tayari.” 

0 comments:

Post a Comment