Monday, July 1, 2013

PREZZO ASEMA WAREMBO MTANITAMBUA!!!!


JACKSON Ngechu Makini ‘CMB Prezzo’ alizaliwa siku ya Jumatano ya Januari 09, mwaka 1980. Ni rapa lejendari wa Kenya ambaye alikuwa mmoja wa mastaa waliowakilisha nchi zao katika Shindano ya Big Brother Africa ‘StarGame’, 2012.

 
CMB Prezzo.
Kama ulikuwa hujui, jamaa alizaliwa katika Jiji la Nairobi miaka 33 iliyopita, alikulia maisha ya kitaani eneo la Eastleigh na atakuwa mmoja wa wanamuziki wakali watakaoshusha bonge la burudani katika Tamasha la Matumani 2013 litakolofunga mitaa ya Jiji la…

JACKSON Ngechu Makini ‘CMB Prezzo’ alizaliwa siku ya Jumatano ya Januari 09, mwaka 1980. Ni rapa lejendari wa Kenya ambaye alikuwa mmoja wa mastaa waliowakilisha nchi zao katika Shindano ya Big Brother Africa ‘StarGame’, 2012.
 
CMB Prezzo.
Kama ulikuwa hujui, jamaa alizaliwa katika Jiji la Nairobi miaka 33 iliyopita, alikulia maisha ya kitaani eneo la Eastleigh na atakuwa mmoja wa wanamuziki wakali watakaoshusha bonge la burudani katika Tamasha la Matumani 2013 litakolofunga mitaa ya Jiji la Dar na viunga vyake kwenye Uwanja wa Taifa, Julai 7, mwaka huu.
Prezzo ni mwanamuziki mkubwa ambaye alianza ‘kuhaso’ katika muziki miaka mingi, alikuja kuwika kwenye miaka ya mwanzoni mwa karne ya 21.
Pamoja na kukumbana na vipingamizi vingi, nyota ilikuja kung’aa baada ya nyimbo zake kukubalika kwa maelfu ya mashabiki wake waliokuwa wakizisikiliza, kuziomba kwenye stesheni mbalimbali za redio na runinga huku wakihudhuria katika matamasha yake ya wazi na klabu.
Albam yake ya kwanza ni Naleta Action aliyoiachia mwaka 2004 ikiwa na ngoma zilizoshika kama Naleta Action, Lets Get Down, Mahangaiko, Leo ni Leo, Mimi na Wewe, Mafans na nyingine zilizobamba.
Katika albam hiyo, jamaa alimshirikisha mama yake ambaye aliimba mistari kadhaa katika moja ya nyimbo zake.
Albam hiyo iliuza nakala nyingi na kumfanya Prezzo kuamini kuwa alishakubali Afrika Mashariki kutokana na aina ya ngoma zake zenye hisia.
Prezzo anajulikana kutokana na aina ya maisha ya gharama anayopendelea kama kuvaa mikufu ya bei ghali, nguo, magari ya vitu vingine vya kitajiri.
poste bywww.Thesuperonenews.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment