SPIKA wa Bunge bi
Anna Makinda amesema wabunge wengi wamepungukiwa uwezo kutokana na
kuacha kuzungumzia mambo muhimu badala yake wanajadili watu binafsi.
Aidha Mbunge wa kuteuliwa James Mbatia (NCCR Mageuzi ) amesema wabunge
wengi ni wafungwa watarajiwa na ameomba magereza yaboreshwe maana wengi
wataenda huko kutokana na kushiriki kushabikia na kupitisha mambo ambayo
hayana maslahi kwa taifa.
“Wabunge tumepungukiwa badala ya
kujadili ishu, sisi tunajadili watu binafsi,” alisema na kuongeza kuwa
suala la wabunge kushambuliana wenyewe si kitu ambacho wananchi wanataka
kukisikia na kusisitiza kuwa walio wengi wamepungukiwa.
Pia alimuomba Waziri wa Elimu na Mafunzo
ya ufundi, Dk Shukuru Kawambwa kuchukua changamoto mbalimbali
zilizojitokeza kwa wizara yake katika michango ya wabunge na kuifanyia
kazi. Mbatia “Wabunge wengi ni wafungwa watarajiwa, naomba magereza
yaboreshwe maana wengi wataenda huko kutokana na kushiriki kushabikia na
kupitisha maambo ambayo hayana maslahi kwa Taifa.
“Ni suala linalosikitisha kuona wabunge
wanakuwa chanzo cha mambo yasiyo na faida, hivyo nawaambia wajiandae,
historia itatuhukumu, ni vyema tukabadilika na kuweka mbele maslahi ya
Taifa badala ya ubinafsi,” alisema Mbatia.
Bajeti kupitiwa Wizara zote
zimekamilisha kazi ya kusoma bajeti zake bungeni na leo Kamati mpya ya
Bunge inayoshughulika mambo ya Bajeti inaanza kazi yake itakapokutana na
mawaziri kwa ajili ya kupitia bajeti ya Serikali.
Kazi za kamati hiyo mpya inayoongozwa na
Mbunge wa Bariadi Magharibi Andrew Chenge itafanya majumuisho
kuzingatia hoja zenye maslahi kwa taifa zilizojitokeza wakati wa
kujadili mapato na matumizi ya wizara mbalimbali.
Miongoni mwa wizara ambazo mapato na
matumizi yake yalipingwa ni Wizara ya Maji ambayo wabunge waliungana
kuikataa hali iliyofanya serikali kwenda kufanya marekebisho. Wizara
hiyo ililalamikiwa na wabunge wengi kwa vile maeneo mengi ya nchi hayana
maji hali inayozua malalamiko kwa wananchi.
Kwa hali hiyo wabunge waligoma kuunga
mkono hoja ya waziri wa maji Profesa Jumanne Maghembe hali ambayo
ilimlazimu kwenda kufanya mabadiliko. Wizara nyingine ambayo wabunge
walichachamaa zaidi ni Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi ambayo
inaelezwa inatengewa fedha kidogo wakati majukumu yake yanamgusa zaidi
mwananchi.
Kutokana na udogo wa bajeti ya wizara
hiyo, mambo mengi yameshindwa kufanyika, wakati sera ya CCM
inaelekezakuwa lengo la Serikali ni kuhuisha ufugaji ili waweze kuwa
wafugaji wa kisasa kuliko ilivyo sasa.
Kwa upande wa Wizara ya Elimu na Mafunzo
ya Ufundi ambayo bajeti yake ilipitishwa juzi, pia baadhi ya wabunge
wamelalamika hatua ya nusu ya bajeti yote kwenda Bodi ya Mikopo ya Elimu
ya Juu huku kiasi kilichobaki, kikitajwa kwamba ni kidogo kisichokidhi
mahitaji.
Bunge ambalo lilianza kikao chake Aprili
8 mwaka huu pamoja na kamati hiyo kuanza kazi yake, leo kutakuwa na
uchaguzi wa wajumbe watakaowakilisha Bunge katika Taasisi/Vyuo
mbalimbali.
Hotuba ya bajeti ya Serikali itasomwa na Waziri wa Fedha William Mgimba Alhamisi ijayo na itajadiliwa kwa siku tano.
0 comments:
Post a Comment