WAAMUZI WATATU WAFUNGIWA MIEZI MITATU
Wakati timu ya Ivory Coast inatarajiwa
kuwasili leo usiku (Juni 13 mwaka huu) kwa ndege maalum, tiketi kwa
ajili ya mechi kati yake na Taifa Stars itakayochezwa Jumapili kwenye
Uwanja wa Taifa zinaanza kuuzwa kesho mchana (Juni 14 mwaka huu) kwenye
vituo mbalimbali jijini Dar es Salaam.
Viingilio katika mechi hiyo ya mchujo ya
Kombe la Dunia, Kanda ya Afrika katika kundi C ni sh. 5,000 kwa viti
vya rangi ya kijani, sh. 7,000 viti vya rangi ya bluu, sh. 10,000 viti
vya rangi ya chungwa, sh. 15,000 VIP C, sh. 20,000 kwa VIP B wakati VIP A
itakuwa sh. 30,000.
Pia viti 100 vilivyo katika sehemu ya
Wageni Maalumu (VVIP) vitauzwa kwa sh. 50,000 kila kimoja. Tiketi hizo
zitauzwa katika ofisi za TFF, na watakaonunua watapewa kadi maalumu
zenye majina yao, majina ambayo pia watayakuta katika vita watakavyokaa.
Kwa maana hiyo hakutakuwa pasi maalumu (free pass) za kuingia VVIP.
PONGEZI KWA RAIS MPYA WA ZFA
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amempongeza Rais mpya wa Chama cha Mpira
wa Miguu Zanzibar (ZFA), Ravia Idarous Faina aliyechaguliwa katika
uchaguzo mdogo uliofanyika hivi karibuni.
Amesema ushindi aliopata Faina
unaonyesha jinsi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa ZFA walivyo na imani naye
katika kuhakikisha maendeleo ya mpira wa miguu visiwani humo.
Rais Tenga amesema ni imani yake kuwa
Rais Faina ataendeleza ushirikiano uliopo kati ya TFF na ZFA kwa ajili
ya ustawi wa mpira wa miguu katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na
kumtakiwa kila kheri katika wadhifa wake huo mpya.
WAAMUZI WATATU WAFUNGIWA MIEZI MITATU
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) limefungia miezi mitatu waamuzi watatu walioshindwa kuchezesha
mechi namba 32 ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) kati ya Mpwapwa Stars
ya Dodoma na Machava FC ya Kilimanjaro iliyokuwa ichezwe Juni 2 mwaka
huu Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
TFF kupitia Kamati yake ya Waamuzi
iliyokutana katika kikao chake cha Juni 12 mwaka huu kupitia taarifa
mbalimbali za waamuzi wa RCL ilibaini makosa yaliyofanywa na baadhi ya
waamuzi na kuyatolea uamuzi.
Waamuzi hao waliofungiwa ambao wanatoka
mkoani Singida ni Jilili Abdallah, Amani Mwaipaja na Theofil Tegamisho.
Wamefungiwa kwa kutoripoti katika kituo walichopangiwa (Uwanja wa
Jamhuri, Dodoma) na kutoa taarifa ya uongo kwa kushirikiana na Kamishna
wa mechi hiyo.
Kanuni iliyotumika kuwafungia ni ya 28
kifungu (d) na (g) ya Ligi za TFF, na adhabu hiyo imeanza Juni 13 mwaka
huu. Waamuzi hao pamoja na kamishna badala ya kwenda Uwanja wa Jamhuri,
wao walikwenda kwenye Uwanja wa Mgambo ulioko Mpwapwa na kuandika ripoti
iliyoonesha kuwa timu ya Machava FC haikufika uwanjani wakati wakijua
kuwa mechi hiyo ilitakiwa kuchezwa katika Uwanja wa Jamhuri.
0 comments:
Post a Comment