POULSEN: “LENGO KUPATA MATOKEO MAZURI
Taifa Stars inatupa karata yake ya pili
ugenini kwenye mechi za mchujo za Kombe la Dunia kwa kesho (Juni 8 mwaka
huu) kuikabili Morocco (Lions of the Atlas) kwenye Uwanja wa Grand
Stade hapa Marrakech, Morocco.
Washabiki wa Morocco wanaonekana
kuikatia tama timu yao yenye pointi mbili tu nyuma ya Ivory Coast
inayoongoza kundi hilo la C ikiwa na pointi saba ikifuatiwa na Tanzania
yenye sita. Huo ni mtazamo wa washabiki, lakini kwa upande wa timu
inaonekana imepania kujichomoa katika nafasi za chini.
Kwa upande wa Kocha wa Stars, Kim
Poulsen amesema timu yake imepania mechi hiyo, lengo likiwa ni kuona
inapata matokeo mazuri baada ya dakika 90 za mechi hiyo itakayokuwa
chini ya refa Daniel Frazier Bennett wa Afrika Kusini.
Amesema timu yake itacheza kwa umakini
na uangalifu kwa vile wanajua wapinzani wao wakicheza mbele ya washabiki
wao watakuwa katika shinikizo za kushinda, jambo ambalo wamejiandaa
kukabiliana nalo.
Kwa upande wa maandalizi, Kim amesema
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na wadhamini wa timu hiyo
Kilimanjaro Premium Lager wameiandaa vizuri kwani iko kambini kwa wiki
tatu sasa na kupata mechi ya kirafiki dhidi ya Sudan iliyochezwa wiki
iliyopita nchini Ethiopia.
Stars iliifunga Morocco mabao 3-1
zilipokutana Machi 24 mwaka huu jijini Dar es Salaa. Lakini zilipokutana
hapa Marrakech mara ya mwisho mwaka 2011, Morocco iliibuka na ushindi
wa mabao 3-1.
Kim amesisitiza kuwa kikosi chake
kimepania kufanya vizuri katika michuano hii ya mchujo ya Kombe la
Dunia, ha hiyo inathibitishwa na matokeo ya timu kadri inavyoendelea
kucheza mechi za mashindano.
“Moja ya mipango yetu katika mechi hizi
za Kombe la Dunia ni kushinda nyumbani, hilo hadi sasa tumelifanya kwa
asilimia 100. Lakini ili tukae vizuri zaidi tumekuja hapa Morocco kwa
lengo la kupata matokeo mazuri, ingawa tunajua mechi itakuwa ngumi,”
amesema kocha huyo raia wa Denmark.
Kwa hapa Marrakech mechi hiyo imekuwa
haizungumzwi mara kwa mara, na kubwa ni kuwa Wamorocco wengi wanaamini
kuwa timu yao ambayo hadi sasa ina pointi mbili haina nafasi ya kusonga
mbele katika hatua inayofuata ya michuano hiyo.
Bonifa
0 comments:
Post a Comment