Nadal ambaye yupo nafasi ya nne kwa sasa katika ubora duniani amemfunga muhispania mwenzake kwa seti 6-3, 6-2,6-3 katika mchezo uliochezwa kwa masaa mawili tu.
Nadal alisema “hii ni moja ya mataji muhimu sana kwangu”
“Napenda kusema asante sana kwa wote waliokuwa na mimi katika kipindi chote na hasa katika mwaka jana ambapo nilikuwa na majeraha”
Katika fainali hiyo alikuwepo mwanariadha maarufu kutoka nchi ya Jamaica Usain Bolt.
0 comments:
Post a Comment