MWAKA JANA ILICHEZWA VILLA PARK!!
MGAO TIKETI: MAN UNITED 35,000 WIGAN 15,000!
MWAKA
HUU, ule mtanange wa ‘Fungua Dimba’ Msimu mpya wa 2013/14 kati ya
Mabingwa wa England, Manchester United, na Washindi wa FA CUP, Wigan
Athletics, utachezwa Uwanja wa Wembley Jijini London hapo Agosti 11
kuanzia Saa 10 Jioni.
Timu zote mbili zitatinga kwenye Mechi
hiyo spesho ya kwanza kabisa kwa Msimu mpya zikiwa na Mameneja wapya kwa
Man United kuongozwa na David Moyes aliemrithi Mstaafu Sir Alex
Ferguson lakini Wigan hadi sasa haina Meneja mpya baada ya kuondokewa na
Roberto Martinez ambae ameenda huko Everton kuchukua wadhifa wa David
Moyes.
Akithibitisha Mechi hii, Katibu Mkuu wa
FA, Alex Horne, alisema: “Inabidi urudi nyuma hadi Mwaka 1985 ili kuiona
Man United wakicheza kwenye Ngao hii bila ya Sir Alex Ferguson! Macho
ya kila Mtu yatakuwa kwa David Moyes akiiongoza Man United kwa mara ya
kwanza!”
Vile vile, Horne alisema kuwa Mechi hii
itakuwa ya mvuto licha ya Wigan Msimu huo mpya kucheza Daraja la chini,
Championship, baada kushuka Daraja toka BPL, Barclays Premier League,
kwa vile tu iliitwanga Man City kwenye Fainali ya FA CUP.
Hata hivyo, kwa kutwaa FA CUP, Wigan imepata nafasi kucheza Ulaya Msimu wa 2013/14 kwenye Mashindano ya UEFA EUROPA LIGI.
Kila Klabu tayari imetengewa Mgao wake
wa Tiketi na Man United watapewa Tiketi 35,000 kuziuza huku Wigan
wakipewa Tiketi 15,000 tu na Bei ya Tiket hizo ni kuanzia Pauni 20 hadi
45 [Shilingi 50,900 hadi 114,500].
Akiongelea Mgao huo wa Tiketi, Horne
alifafanua: “Washabiki wa Manchester United wanasafiri kwa wingi mno na
mgao wa Wigan umefuatia mahudhurio ya Washabiki wao katika Mechi mbili
walizocheza Uwanja wa Wembley kwenye FA CUP Msimu uliopita.”
WASHINDI WALIOPITA:
MWAKA
|
TIMU |
2012
|
Manchester City |
2011
|
Manchester United |
2010
|
Manchester United |
2009
|
Chelsea FC |
2008
|
Manchester United |
2007
|
Manchester United |
2006
|
Liverpool FC |
2005
|
Chelsea FC |
2004
|
Arsenal FC |
2003
|
Manchester United |
2002
|
Arsenal FC |
2001
|
Liverpool FC |
2000
|
Chelsea FC |
1999
|
Arsenal FC |
1998
|
Arsenal FC |
1997
|
Manchester United |
1996
|
Manchester United |
1995
|
Everton FC |
1994
|
Manchester United |
1993
|
Manchester United |
1992
|
Leeds United |
1991
|
Tottenham Hotspur |
1991
|
Arsenal FC |
1990
|
Liverpool FC |
1990
|
Manchester United |
1989
|
Liverpool FC |
1988
|
Liverpool FC |
1987
|
Everton FC |
1986
|
Liverpool FC |
1986
|
Everton FC |
1985
|
Everton FC |
1984
|
Everton FC |
1983
|
Manchester United |
1982
|
Liverpool FC |
1981
|
Tottenham Hotspur |
1981
|
Aston Villa |
1980
|
Liverpool FC |
1979
|
Liverpool FC |
1978
|
Nottingham Forest |
1977
|
Liverpool FC |
1977
|
Manchester United |
1976
|
Liverpool FC |
1975
|
Derby County |
1974
|
Liverpool FC |
1973
|
Burnley FC |
1972
|
Manchester City |
1971
|
Leicester City |
1970
|
Everton FC |
1969
|
Leeds United |
1968
|
Manchester City |
1967
|
Manchester United |
1967
|
Tottenham Hotspur |
1966
|
Liverpool FC |
1965
|
Liverpool FC |
1965
|
Manchester United |
1964
|
West Ham United |
1964
|
Liverpool FC |
1963
|
Everton FC |
1962
|
Tottenham Hotspur |
1961
|
Tottenham Hotspur |
1960
|
Wolverhampton Wanderers |
1960
|
Burnley FC |
1959
|
Wolverhampton Wanderers |
1958
|
Bolton Wanderers |
1957
|
Manchester United |
1956
|
Manchester United |
1955
|
Chelsea FC |
1954
|
Wolverhampton Wanderers |
1954
|
West Bromwich Albion |
1953
|
Arsenal FC |
1952
|
Manchester United |
1951
|
Tottenham Hotspur |
1950
|
England |
1949
|
Wolverhampton Wanderers |
1949
|
Portsmouth FC |
1948
|
Arsenal FC |
1938
|
Arsenal FC |
1937
|
Manchester City |
1936
|
Sunderland AFC |
1935
|
Sheffield Wednesday |
1934
|
Arsenal FC |
1933
|
Arsenal FC |
1932
|
Everton FC |
1931
|
Arsenal FC |
1930
|
Arsenal FC |
1929
|
English Professionals |
1928
|
Everton FC |
1927
|
Cardiff City |
1926
|
English Amateurs |
1925
|
English Amateurs |
1924
|
English Professionals |
1923
|
English Professionals |
1922
|
Huddersfield Town |
1921
|
Tottenham Hotspur |
1920
|
West Bromwich Albion |
1913
|
English Professionals |
1912
|
Blackburn Rovers |
1911
|
Manchester United |
1910
|
Brighton & Hove Albion |
1909
|
Newcastle United |
1908
|
Manchester United |
0 comments:
Post a Comment