skip to main |
skip to sidebar
Mkoani Arusha hali sio shwari!!!!

Arusha.
Katika mkusanyiko huo kuna Askari Polisi mmoja ambae alijichanganya na kuingia
katikati ya wafuasi wa Chadema ambao walikua wanasubiri kujua utaratibu
wa kuaga miili ya Marehemu waliolipuliwa kwa mabomu na kufariki June 15
2013 na wengine zaidi ya 70 kujeruhiwa.
Baada ya hapo hawa Wafuasi hawakupenda kitendo cha Polisi
kujichanganya nao hivyo ikazuka kama kutoelewana huku wakitaka atoke,
baada ya dakika kadhaa huku pia Viongozi wa Chadema wakihutubia…. ndio
mabomu yakaanza kusikika.
Lakini pia “Baada ya Tundu Lissu wa Chadema
kuhutubia na kusema chanzo cha vifo vya June 15 2013 ni Polisi, yani
vifo hivyo viliratibiwa na RPC Arusha… mabomu ya machozi ndio yakaanza
kulipuliwa”
Mpaka mida ya saa kumi na moja
wafuasi wa Chadema bado wako maeneo ya Soweto Arusha, wamegoma kuondoka
na kusema wanataka kujua kwanza usalama wa Viongozi wao…. lakini pia
mabomu yanaendelea kusikika kwenye sehemu nyingine kama Sanawari, Arusha
mjini, Mianzini na maeneo mengine.www.Thesuperonenews.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment