Saturday, June 1, 2013

MIKOVILLA NA SINZA NGOMA DROO




Mikovilla leo wamelazimishwa sare ya goli 2-2 na Sinza Boy, mchezo uliochezwa katika uwanja shule ya msingi ushindi ulipo Mikocheni B jijini Dar es salaam.
Sinza boy walikuwa wa mwanzo kufika langoni mwa Mikovilla lakini wakishindwa kudumbukiza mpira kwenye nyavu za Mikovilla.
WACHEZAJI WA MIKOVILLA WAKIENDA MAPUMZIKO

Mikovilla wakionekana wakicheza bila mshambuliaji katika dakika 15 za mwanzo, wakiwa wamejazana katikati mwa uwanja hivyo kualimbu mipango ya Sinza boys, na kupelekea kuonekana kuna ugumu kwao kupata goli.

Mikovila waliandika goli la kuongoza kupitia kwa Kiangio akiunga mpira wa Mada na kupelekea Mikovilla kuanza kucheza mpira huku Sinza boy wakitumia mipira ya kushtukiza, na mpaka timu zina kwenda mapumziko, Mikovilla walikuwa mbele kwa goli 1-0.


Katika kipindi cha pili Mikovila walifanya mapandiliko, ambayo yalipelekea Lase ‘Chuji’ kuingia kati akitokea pembeni alipo kuwa anacheza kipindi cha kwanzana kupelekea mipira kwenda mbele kiuhakika zaidi na kuwanyima utulivu mabeki wa Sinza Boy.
Katika dakika ya 55 Annuari aliwasawazishia Sinza Boy akitu,ia udhaifu wa mabeki wa Mikovilla na kupelekea mchezo kuwa wakushambuliana kwa zamu.
Uelewano mzuri kati ya Lase na Kiangio kulipelekea Mikovila kupata kugoli la pili likifungwa na Kiangio akimalizia mpira pasi murua ya dogo Lase.

Wakati Mikovila wakijiamini wametoka na ushindi hii leo, uku wakianza kuwapumzisha baadhi ya nyota wao akiwemo Kiangio, walijikuta katika wakati mgumu katika dakika 15 za mwisho.

Sinza Boy walilisakama vilivyo lango la Mikovilla huku John ‘Ngassa’ akiwa mwiba kwa mabeki wa Mikovilla.

John aliipatia goli la kusawazisha Sinza boy akimalizia mpira mrefu uliopigwa, huku mabeki wa Mikovilla wakimtengenezea mazingira ya kuzidi na kupelekea kubakia yeye na kipa na kufunga goli la kusawazusha.
Kuingia kwa goli hilo kulipelekea wachezaji wa Mikovilla kwenda kumvaa Mwamuzi, wakilalamika kuwa mfungaji alikuwa ameotea, na kutaka kuvunja mchezo.

Kuingia kwa goli hilo kulipelekea Sinza boy kutawala mchezo na kuendelea kulisakama lango la Mikovilla,na mpaka mwisho wa mchezo Mikovilla 2-2 Sinza boy.
WACHEZAJI WA SINZA BOYS WAKIMSIKILIZA KOCHA WAO 

MCHEZAJI WA SINZA BOY

WACHEZAJI WA MIKOVILLA WAKIMSIKILIZA KOCHA WAO

0 comments:

Post a Comment