Wednesday, June 5, 2013

MASHINDANO YA KAGAME CUP YAKIWA YANAKALIBIA YANGA NA SIMBA WAKABIDHIWA VIFAA KWA AJILI YA MICHUANO HIYO


Kutoka kushoto ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro George Kavishe, Baraka Kizuguto , Geofrey Makau na Lawrence Mwalusako Katibu Mkuu wa Yanga wakionyesha vifaa walivyokabidhiwa na kampuni ya bia nchini TBL
Wadhamini wa klabu ya Young Africans Sports Club kampuni ya TBL kupitia kinywaji chake cha Kilimanjaro leo imekabidhi vifaa kwa ajili ya mashindano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati maarufu kama kombe la Kagame inayotazamiwa kuanza Juni 18 mwaka huu nchini Sudan.
Akikabidhi vifaa hivyo Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alisema, ‘‘ Bila ubishi Yanga na Simba ndio klabu kubwa za mpira Tanzania na zote zimefika  katika fainali za mchuano wa Kombe la Kagame kwa mara ya  19 sasa, haya ni mafanikio makubwa kwa hizi timu, kama wadhamini wakuu wa timu hizi, Kilimanjaro Premium Lager  inaziunga mkono Simba na Yanga katika harakati zao kucheza tena fainali za michuano hii ya kusisimua na ya kihistoria.
Aliongeza kuwa  Kombe la Kagame ni mashindano makubwa Africa mashariki na kati, na ni jukwaa bora kwa wachezaji wetu kuonyesha vipaji vyao  dhidi ya wachezaji wa viwango vya juu katika kanda hii lakini pia ni jukwaa zuri kwa wale wanaounda timu za taifa kuchagua wachezaji.
“Ushirikiano huu baina ya Bia ya Kilimanjaro na klabu hizi ni mizizi inayotokana na maadili katika kazi, kufanya kazi kama timu na ile kiu ya mafanikio.  Na mafanikio ya ushirikiano huu ni pamoja na kushuhudia  mara kwa mara timu hizi mbili zikitoa  wachezaji  kwa timu ya Taifa  (Taifa Stars) ambao  wamekuwa na matokeo mazuri chini ya udhamini wa Bia ya Kilimanjaro.
Tutaendelea  kusaidia  timu hizi, na kuhakikisha tunapeleka mpira wa nchi hii kwenye kilele cha mafanikio. 
Meneja wa Bia ya Kilimanjaro pia aliwataka  Simba na Yanga kuhakikisha wanaiwakilisha nchi yetu vizuri  katika mchuano huu mkubwa wa vilabu katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na kuwasihi kuchukua  ushindi na kurudi na kombe la 12 la Kagame kwa mashabiki wanaosubiria kwa hamu
Akiongea kwa niaba ya klabu ya Yanga, Katibu Mkuu Lawrence Mwalusako aliwashukuru TBL kupitia kinywaji chake cha Kilmanjaro kwa udhamini wanaoutoa kwa timu yake, kwani wanajivunia kuwa na wadhamini bora ambao wanawafanya kuweza kufanya vizuri katika michezo na kuahid kuendeleza kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali.

0 comments:

Post a Comment