Brazil v Japan [-Estadio Nacional de Brasilia - Brasilia
Mashindano haya yanashirikisha Timu 8
ambazo ni Mabingwa wa Mabara yao pamoja, Mwenyeji Brazil na Bingwa
Mtetezi wa Dunia lakini Ulaya itawakilishwa na Timu mbili, Spain na
Italy, kwa vile Spain ndie Bingwa wa Dunia na pia Bingwa wa Ulaya hivyo
nafasi yake kama Bingwa wa Ulaya kuchukuliwa na Italy ambao ndio
Washindi wa Pili wa EURO 2012.
Wakati Mashindano yanaanza Jumamosi Juni
15, Kambi ya Brazil imekumbwa na kizaazaa kuhusu Mpira maalum
uliotengenezwa na Kampuni ya Adidas, uliopewa Jina la CAFUSA, kutumika
wakati Timu ya Taifa ya Brazil Mipira yake rasmi ni ile inayotengenezwa
na Nike na ni hiyo wamekuwa wakiitumia kwenye Mechi zao zote na Mazoezi
yao.
Shirikisho la Soka la Brazil, likipinga
tuhuma kuwa Wadhamini wao wameilazimisha kutumia Mpira wa Nike kwa
limetamka tayari Kambi ya Mazoezi ya Brazil imekuwa ikiutumia Mpira wa
Adidas, CAFUSA.
CAFUSA ni kifupi cha Carnaval, Futebol
na Samba vitu ambavyo ni vpenzi sana vya Wabrazil, Carnaval ikiwa ni
aina ya Ngoma ya Maandamano Mitaani, Futebol ni Soka na Samba ni aina ya
Muziki umaopendwa huko Brazil.
CAFUSA ni mwepesi sana na una mabaka ya Rangi za Bendera ya Brazil.
Baada ya kufanya Mazoezi kadhaa na
CAFUSA, hasa upigaji krosi na frikiki, baadhi ya Wachezaji wa Brazil
waliongelea kuhusu Mpira huo na Straika Fred alisema: “Kwa sisi
Mastraika ni Mpira murua. Ukipiga shuti Mpira unakatika na kuyumba njia
tatu tofauti na kutinga wavuni! Makipa wataumia!”
MFUMO & RATIBA:
MAKUNDI:
KUNDI A:
-Brazil
-Japan
-Mexico
-Italy
KUNDI B:
-Spain
-Uruguay
-Tahiti
-Nigeria
VIWANJA:
-Estadio Mineirao - Belo Horizonte
-Estadio Nacional de Brasilia - Brasilia
-Estadio Castelao - Fortaleza
-Arena Pernambuco - Recife
-Estadio Do Maracana - Rio de Janeiro
-Arena Fonte Nova - Salvador
RATIBA:
JUNI 15
Saa 4 Usiku
Brazil v Japan [Brasilia]
JUNI16
Saa 4 Usiku
Mexico v Italy [Rio De Janeiro]
Saa 7 Usiku
Spain v Uruguay [Recife]
JUNI 17
Saa 4 Usiku
Tahiti v Nigeria [Belo Horizonte]
JUNI 19
Saa 4 Usiku
Brazil v Mexico [Fortaleza]
Saa 7 Usiku
Italy v Japan [Recife]
JUNI 20
Saa 4 Usiku
Spain v Tahiti [Rio De Janeiro]
Saa 7 Usiku
Nigeria v Uruguay [Salvador]
JUNI 22
Saa 4 Usiku
Japan v Mexico [Belo Horizonte]
Italy v Brazil [Salvador]
JUNI 23
Saa 4 Usiku
Nigeria v Spain [Fortaleza]
Uruguay Tahiti [Recife]
NUSU FAINALI
JUNI 26
[Belo Horizonte]
[SAA 4 USIKU]
Mshindi A v Mshindi wa Pili B
JUNI 27
[Fortaleza]
[SAA 4 USIKU]
Mshindi B v Mshindi wa Pili A
MSHINDI WA TATU
JUNI 30
[Salvador]
[SAA 1 USIKU]
FAINALI
JUNI 30
[Rio De Janeiro]
[SAA 7 USIKU]
0 comments:
Post a Comment