Rais wa Misri Mohammed Morsi
amesema kuwa taifa lake litatumia kila mbinu kuhakikisha kuwa Ethiopia
inasitisha ujenzi wa bwawa la maji katika mto Nile .
Idadi kubwa ya raia wa Misri millioni 84 imekuwa ikitegemea mto huo kwa maji safi.
Akishangiliwa na wafuasi wake ,Morsi amesema kuwa ijapokuwa Misri haitaki vita haitokubali usalama wake wa maji kuingiliwa kivyovyote.
Tayari kiongozi huyo anapanga kumtuma waziri wake wa maswala ya kigeni nchini Ethiopia ili kuanzisha mazungumzo kuhusiana na swala hilo.
Misri ina wasiwasi kuwa maji ya mto Nile huenda yakapungua kwa kiwango kikubwa iwapo bwawa hilo litajengwa.
Inasema kuwa, kwa mujibu wa sheria zilizowekwa na mkoloni, ndio taifa linalopaswa kufaidika pakubwa na maji hayo swala linalopingwa na Ethiopia ambayo inasema sheria hiyo imepitwa na wakati.
0 comments:
Post a Comment