
Ingawa Messi alijumuishwa kwenye Kikosi
cha Argentina kwa ajili ya Mechi zao mbili za Mwezi huu za Mchujo za
kuwania kucheza Fainali za Kombe la Dunia, Mchezaji huyo alizikosa Mechi
kadhaa za Klabu yake Barcelona walipokuwa wakimalizia Msimu wao wa La
Liga baada ya kusumbuliwa na tatizo la Musuli za Pajani.
Mara baada ya leo Argentina kucheza na Colombia itafuatia Mechi na Ecuador hapo Jumanne.
Akifafanua, Sabella alisema: "Mguu wake
uko safi. Anaonekana ni mwepesi na yuko tayari kukabiliana na Mabeki
lakini inabidi tuangalie kama yuko fiti baada ya kukaa nje kwa muda
mrefu!”
Ikiwa Messi hatacheza, anaweza
kubadilishwa na Mchezaji wa AS Roma, Erik Lamela au Walter Montillo wa
Klabu ya Brazil, Santos, ambao watatoa sapoti kwa Mastraika wao wa
kawaida Sergio Aguero wa Manchester City na Gonzalo Higuain wa Real
Madrid.
Argentina wako Pointi 4 mbele ya
Ecuador, waliocheza Mechi moja pungufu, na Pointi 5 mbele ya Timu ya 3
Colombia inayoongozwa na Straika hatari Radamel Falcao aliekuwa Atletico
Madrid na sasa yuko Monaco ya France.
Colombia wako chini ya Kocha kutoka
Argentna, Jose Pekerman, ambae ndie alieipeleka Argentina Fainali za
Kombe la Dunia za Mwaka 2006.
RATIBA
[Saa ni za Bongo, Kwenye Mabano Matokeo Mechi za Kwanza]
Ijumaa Juni 7
23:00 Bolivia v Venezuela [0-1]
Jumamosi Juni 8
01:05 Argentina v Colombia [2-1]
01:10 Paraguay v Chile [0-2]
03:10 Peru v Ecuador [0-2]
Jumanne Juni 11
23:30 Colombia v Peru [1-0]
00:00 Ecuador v Argentina [0-4]
Jumatano Juni 12
01:00 Venezuela v Uruguay [1-1]
01:30 Chile v Bolivia [2-0]
Jumapili Septemba 8
01:00 Colombia v Ecuador [0-1]
01:00 Chile v Venezuela [2-0]
01:00 Paraguay v Bolivia [1-3]
01:00 Peru v Uruguay [2-4]
MSIMAMO:
NA |
TIMU |
P |
W |
D |
L |
F |
A |
GD |
PTS |
1 |
Argentina |
11
|
7
|
3
|
1
|
24 |
8 |
16 |
24 |
2 |
Ecuador |
10
|
6
|
2
|
2
|
16 |
10 |
6 |
20 |
3 |
Colombia |
10
|
6
|
1
|
3
|
19 |
7 |
12 |
19 |
4 |
Chile |
11
|
5
|
0
|
6
|
16 |
19 |
-3 |
15 |
5 |
Venezuela |
11
|
4
|
3
|
4
|
9 |
12 |
-3 |
15 |
6 |
Uruguay |
11
|
3
|
4
|
4
|
17 |
21 |
-4 |
13 |
7 |
Peru |
10
|
3
|
2
|
5
|
11 |
15 |
-4 |
11 |
8 |
Bolivia |
11
|
2
|
3
|
6
|
13 |
20 |
-7 |
9 |
9 |
Paraguay |
11
|
2
|
2
|
7
|
8 |
21 |
-13 |
8 |
**FAHAMU: Timu 4 za Juu
zitafuzu moja kwa moja kucheza Fainali za Kombe la Dunia 2014 huko
Brazil na Timu ya 5 itakwenda kucheza Mechi ya Mchujo na Timu kutoka
Kanda ya ASIA kupata Timu 1 ya kuingia Fainali.
0 comments:
Post a Comment