Tuesday, June 18, 2013

KOMBE LA DUNIA 2014: LEO AUSTRALIA, IRAN & SOUTH KOREA ZATINGA BRAZIL!

BRAZIL_2014_BESTBARA LA ASIA limekamilisha idadi yao ya Timu 4 ambazo zitakwenda moja kwa moja Brazil kucheza Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2014 kwa leo Australia, Iran na South Korea kuungana na Japan waliofuzu tangu Wiki 2 zilizopita.
Iran ndio walimaliza wakiwa Vinara wa Kundi A na kufuatiwa na South Korea na toka Kundi B ni Japan waliokuwa Vinara na Australia kushika nafasi ya Pili baada ya leo kuifunga Iraq Bao 1-0 huko Mjini Sydney, Australia huku Bao la ushindi ambalo ndilo limewapa Nafasi ya Pili likifungwa katika Dakika ya 84 na Josh Kennedy alieingizwa kumbadili Mkongwe Tim Cahill katika Dakika ya 77.
KOMBE LA DUNIA 2014-Timu zilizofuzu kucheza Fainali Brazil:
-Brazil (Wenyaji)
-Japan (Asia-Mshindi Kundi B)
-Australia (Asia-Mshindi  wa Pili Kundi B)
-Iran (Asia-Mshindi Kundi A)
-South Korea (Asia-Mshindi wa Pili Kundi B)
Japan walitwaa Ushindi wa Kundi B, na hivyo kuwa Nchi ya kwanza kufuzu kwenda Brazil, hapo Juni 4 walipotoka sare 1-1 na Australia.
Katika Mechi nyingine za Kundi A zilizochezwa leo, Iran waliifunga South Korea 1-0 na Uzbekistan wamekamata nafasi ya 3 baada ya kuinyuka Qatar Bao 5-1 na hivyo wanasubri kucheza na Mshindi wa 3 toka Kundi B ambae atakuwa ama Oman au Jordan wanaocheza baadae leo.
Mshindi wa Mechi ya Uzbekistan v Oman au Jordan atacheza na Timu itakayomaliza Nafasi ya 5 toka Kundi la Nchi za Marekani ya Kusini ili kupata Mshindi atakaekwenda Brazil.
RATIBA/MATOKEO:
Jumanne Juni 18
[Saa ni za Bongo, Kwenye Mabano Matokeo Mechi za Kwanza]
Australia 1 Iraq 0
South Korea 0 Iran 1
Uzbekistan 5 Qatar 1
19:00 Jordan v Oman [1-2]
www.Thesuperonenews.blogspot.com
KUNDI A
NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1
Iran
8
5
1
2
8
2
6
16
2
South Korea
8
4
2
2
13
7
6
14
3
Uzbekistan
8
4
2
2
11
6
5
14
4
Qatar
8
2
1
5
5
13
-8
7
5
Lebanon
8
1
2
5
3
12
-9
5
KUNDI B
NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1
Japan
8
5
2
1
16
5
11
17
2
Australia
8
3
4
1
12
7
5
13
3
0man
7
2
3
2
7
9
-2
9
4
Jordan
7
2
1
4
6
16
-10
7
5
Iraq
8
1
2
5
4
8
-4
5

0 comments:

Post a Comment