Thursday, June 6, 2013

KIKOSI CHA EURO U-21YA ENGLAND CHAANZA VIBAYA BAADA YA KUCHEZEA KICHAPO CHA 1-O DHIDI YA ITARY HUKO ISRAEL

2013_UEFA_European_Under-21_Football_ChampionshipBAO la Dakika ya 79 la frikiki ya Lorenzo Insigne limewapa ushindi Italy wa Bao 1-0 dhidi ya England katika Mechi ya KUNDI A la MASHINDANO YA UEFA kwa ajili ya Vijana wa chini ya Miaka 21 kuwania Ubingwa wa Ulaya, EURO U-21, yaliyoanza hiyo Jana huko Israel.
Katika Mechi ya utangulizi, pia ya KUNDI A, Wenyeji Israel walitoka sare ya Bao 2-2 na Norway.
Katika Mechi ya England na Italy, Craig Dawson alifanikiwa kuifungia England Bao katika Dakika ya 48 lakini Refa Antony Gautier kutoka France alilikataa kwa madai Steven Caulker alisukuma kabla ya kufunga wakati tayari Ubao wa Magoli hapo Uwanjani ushaandika ni Bao kwa England na Mtangazaji hapo Uwanjani kutangaza ni Goli kwa England.
Refa huyo pia alitoa maamuzi tata kadhaa ikiwemo hata hiyo frikiki iliyozaa Bao la Italy kwani awali aliashiria ni Penati na baadae kugeuka na kuonyesha ni frikiki.
VIKOSI:
ENGLAND: Butland, Clyne, Caulker, Dawson, Robinson, Henderson, Lowe, Shelvey (McEachran - 75' ), Redmond, Sordell (Chalobah - 65' ), Wickham (Delfouneso - 82' )
Akiba: Steele, Rudd, Smith, Wisdom, Lees, Chalobah, McEachran, Lansbury, Zaha, Delfouneso
ITALY: Bardi, Donati, Biraghi, Caldirola, Bianchetti, Verratti, Florenzi, Marrone (Rossi - 86' ), Immobile (Gabbiadini - 60' ), Insigne, Borini (Destro - 78' )
Akiba: Colombi, Leali, Capuano, Regini, Sansone, Bertolacci, Saponara, Rossi, Crimi, Gabbiadini, Destro, Paloschi
RATIBA/MATOKEO:
(SAA za BONGO)
KUNDI A:
Israel 2 Norway 2 (5 June, Netanya,)
England 0 Italy 1 (5 June, Tel Aviv,)
England v Norway (8 June, Petah Tikva, 19:00)
Italy v Israel (8 June, Tel Aviv, 21:30)
Israel v England ( 11 June, Jerusalem, 19:00)
Norway v Italy (11 June, Tel Aviv, 19:00)
KUNDI B:
Spain v Russia (6 June, Jerusalem, 19:00)
Netherlands v Germany (6 June, Petah Tikva, 21:30)
Netherlands v Russia (9 June, Jerusalem, 19:00)
Germany v Spain (9 June, Netanya, 21:30)
Spain v Netherlands (11 June, Petah Tikva, 19:00)
Russia v Germany (11 June, Netanya, 19:00)
NUSU FAINALI:
Winner Group B v runner-up Group A (15 June, Netanya, 18:30)
Winner Group A v runner-up Group B (15 June, Petah Tikva, 21:30)
FAINALI:
18 June, Jerusalem, 19:00
DONDOO MUHIMU:
-Wachezaji wanaoruhuiwa kushiriki Mashindano haya ni wale waliozaliwa Tarehe 1 Januari 1990 au baada ya hapo.

0 comments:

Post a Comment