Wednesday, June 12, 2013

EUR0 U-21: ENGLAND AIBU, YAPIGWA MECHI ZOTE, YAFUNGASHA VIRAGO!

ITALY, NORWAY ZAUNGANA NA NETHERLANDS, SPAIN NUSU FAINALI!!
2013_UEFA_European_Under-21_Football_ChampionshipEngland, ambao walishaaga Mashindano ya UEFA kwa ajili ya Vijana wa chini ya Miaka 21 kuwania Ubingwa wa Ulaya, EURO U-21, baada ya Mechi zao 2 za kwanza za KUNDI A, leo wamemaliza michuano hiyo kwa aibu kubwa baada ya kufungwa Mechi yao ya mwisho Bao 1-0 na Wenyeji Israel.
Katika Mechi nyingine ya KUNDI A iliyochezwa pia leo, Italy na Norway zilitoka Sare ya Bao 1-1 na wote kutinga Nusu Fainali ambayo watacheza na Mabingwa Watetezi Spain na Netherlands ambao wamefuzu toka KUNDI B wakiwa na Mechi moja mkononi.
Bao lililoiua England leo lilifungwa na Ofir Kriaf katika Dakika ya 80 na kuiacha England ikimaliza Mashindano hayo ikishika mkia.
KUNDI A
[Timu zimemaliza Mechi zao zote 3]
Italy Pointi 7
Norway 5
Israel  4
England 0
Matokeo ya michuano hii yameacha hatima ya Kocha wa England, Stuart Pearce, kwenye utata ingawa mwenyewe alishajitetea kwamba Timu yake kuwakosa Mastaa wakubwa kina Oxlade-Chamberlain, Phil Jones, na wengine ambao walikuwa na Kikosi cha Kwanza cha Timu ya England imewaathiri lakini hata hivyo walikuwepo kina Wilfried Zaha, Thomas Ince, Henderson, Caulker na Njonjo.
KUNDI B
[Timu zimecheza Mechi 2 bado 1]
Netherlands Pointi 6
Spain 6
Germany 0
Russia 0
Kesho KUNDI B linamaliza Mechi zake kwa Netherlands na Spain, ambazo zimeshatinga Nusu Fainali, kupambana ili kupata ipi ya kwanza huku Germany ikicheza na Russia, Mechi ya kukamilisha Ratiba tu kwani wote wameshafungasha virago.
RATIBA/MATOKEO:
(SAA za BONGO)
KUNDI A:
Israel 2 Norway 2 (5 June)
England 0 Italy 1 (5 June)
England 1 Norway 3 (8 June)
Italy 4 Israel (8 June)
Israel 1 England 0 ( 11 June)
Norway v Italy (11 June)
KUNDI B:
Spain 1 Russia 0 (6 June)
Netherlands 3 Germany 2 (6 June)
Netherlands 5 Russia 1 (9 June)
Germany 0 Spain 1 (9 June)
Spain v Netherlands (11 June, Petah Tikva, 19:00)
Russia v Germany (11 June, Netanya, 19:00)
NUSU FAINALI:
Mshindi Kundi B v Norway (15 Juni, Netanya, 18:30)
Italy v Mshindi wa Pili Kundi B (15 Juni, Petah Tikva, 21:30)
FAINALI:
18 June, Jerusalem, 19:00
DONDOO MUHIMU:
-Wachezaji wanaoruhuiwa kushiriki Mashindano haya ni wale waliozaliwa Tarehe 1 Januari 1990 au baada ya hapo.
WASHINDI WALIOPITA:
2011: Spain
2009: Germany
2007: Netherlands
2006: Netherlands
2004: Italy
2002: Czech Republic
2000: Italy
1998: Spain
1996: Italy
1994: Italy
1992: Italy
1990: USSR
1988: France
1986: Spain
1984: England
1982: England
1980: USSR
1978: Yugoslavia
WACHEZAJI BORA WA MASHINDANO YALIYOPITA:
2011: Juan Mata (Spain)
2009: Marcus Berg (Sweden)
2007: Rosyton Drenthe (Netherlands)
2006: Klaas Jan Huntelaar (Netherlands)
2004: Alberto Gilardino (Italy)
2002: Petr Cech (Czech Rep)
2000: Andrea Pirlo (Italy)
1998: Francesc Arnau (Spain)
1996: Fabio Cannavaro (Italy)
1994: Luis Figo (Portugal)
1992: Renato Buso (Italy)
1990: Davor Suker (Croatia)
1988: Laurent Blanc (France)
1986: Manuel Sanchis (Spain)
1984: Mark Hateley (England)
1982: Rudi Voeller (Germany)
1980: Anatoli Demianenko (USSR)
1978: Vahid Halilhodzic (Yugoslavia)

0 comments:

Post a Comment