Friday, June 14, 2013

CLABU YA ASERNAL NCHINI UINGEREZA YAMPA SIR CHIPS KESWICK! MAJUKUMU MAPYA

PELLEGRINI MENEJA MPYA CITY, ARSENAL YAPATA MWENYEKITI MWINGINE

PELLEGRINIWAKATI Manchester City ikithbitisha kuwa Manuel Pellegrini ndie Meneja wao mpya, huko London Klabu ya Arsenal imetangaza Mwenyekiti wao mpya ni Sir Chips Keswick.
Manuel Pellegrini
Manuel Pellegrini, Raia wa Chile ambae alikuwa Kocha wa Malaga ya Spain, amethibitishwa kuwa ndie Meneja mpya wa Manchester City na kupewa Mkataba wa Miaka mitatu.
+++++++++++++++++++++++++
WASIFU: Manuel Pellegrini
-Akiwa Beki, alicheza Soka lake lote huko kwao Chile na Klabu ya Universidad Chile na kucheza Mechi 450
-Alistaafu Mwaka 1986 na kuanza Umeneja Klabu ya Palestino Mwaka 1987
-Kama Meneja ameshaongoza Klabu 10 ikiwa ni pamoja na Villarreal (2004-09), Real Madrid (2009-10) na sasa Malaga
-Ametwaa Ubingwa akiwa Meneja huko Nchini Ecuador na Argentina na kunyakua Intertoto Cup na Villarreal Mwaka 2004
Pellegrini, Mwenye Miaka 59, anamrithi Roberto Mancini alietimuliwa Mwezi Mei.
Akiwa na Malaga, Pellegrini aliisaidia Klabu hiyo ya Spain kufuzu kuingia UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI walipofanya vyema kwenye Msimu wa 2011/13 wa La Liga na Msimu uliofuata, wa 2012/13, walishiriki UCL na kufika Robo Fainali.
Akitokea huko Marekani ya Kusini, Pellegrini alitua Spain Mwaka 2004 kuifundisha Villareal na Mwaka 2009 kutua Real Madrid lakini baada ya Msimu mmoja, akiiongoza Timu iliyokuwa na Mastaa wapya kina Cristiano Ronaldo, Karim Benzema na Xabi Alonso haikufua dafu na kumaliza ya Pili, na yeye kutimuliwa.
Pellegrini anakuwa Meneja wa 3 kwa Man City tangu inunuliwe na Abu Dhabi United Group hapo Mwaka 2008 wengine wakiwa ni Mark Hughes na Roberto Mancini.
Arsenal: Mwenyekiti mpya ni Sir Chips Keswick kumbadili Peter Hill-Wood
Arsenal imemteua Sir Chips Keswick kama Mwenyekiti wao kuchukua nafasi ya Peter Hill-Wood alieachia ngazi kwa sababu za kiafya.
Hill-Wood, Miaka 77, anaachia ngazi baada ya Miaka 51 akiwa kwenye Bodi ya Klabu hiyo.
Hill-Wood amekuwa Mwenyekiti wa Arsenal tangu 1982, wakati Babu yake, Sir Samuel, na Baba yake Mzazi, Denis, walikuwa ni Wenyeviti waliomtangulia katika himaya iliyoanza Mwaka 1927.
Sir Chips Keswick, ni Mkurugenzi wa Bank of England, na amekuwa kwenye Bodi ya Arsenal tangu Mwaka 2005.Thesuperonenews.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment