Klabu za Manchester United na Arsenal
zimeingia kwenye vitakali ya kuwania saini ya kiungo wa kimataifa wa
Hispania Cesc Fabregas anawaniwa na klabu za Manchester United na
Arsenal baada ya klabu yake ya Fc Barcelona kudaiwa kuwa tayari
kusikiliza ofa kwa ajili yake .
Fabregas ambaye alicheza nchini England kwenye klabu ya Arsenal kwa
muda wa miaka nane ameshindwa kufikia kiwango kilichotarajiwa na
Barcelona wakati inamnunua toka Arsenal na kwa sasa iko tayari kumuuza
ili kutengeneza fedha za kununua mchezaji mwingine .
Kocha mpya wa Manchester United David Moyes amegundua kuwa United ina
tatizo kwenye safu ya kiungo na yuko tayari kuidhinisha paundi milioni
40 kumnunua Cesc , hata hivyo Arsenal ndio wenye haki ya kwanza ya
kuzungumza na kiungo huyo kwa mujibu wa makubaliano baina ya Barca na
Arsenal wakati wa mauzo yake toka London kwenda Hispania na endapo
watakuwa tayari kumnunua basi Unitd wanaweza kupoteza nafasi ya
kumsajili.
Kwa upande mwingine kocha wa Arsenal Arsene Wenger hapo jana alianza
rasmi mchakato wa usajili kwenye kikosi chake baada ya kutuma ofa ya
paundi milioni 22 kwa ajili ya kiungo wa Everton Marouanne Fellaini .
United nao wanajiandaa kumthibitisha beki wa timu ya taifa ya Uruguay
kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 na klabu ya Penarol Guillermo
Varela ambaye alithibitisha mwenyewe kufanyiwa vipimo vya afya huko
Manchester.
0 comments:
Post a Comment