
"Balotelli ni mchezaji mkubwa, ingawa ni mtu wa vurugu," alisema Bolt. "Hajawahi kukosa penati. Nimekutana nae mara kadhaa na kiukweli sina mapenzi nae sana."
Balotelli akajibu kupitia akaunti yake rasmi ya "@usainbolt get to no people before to judge them! Isnt very kind what u said about me..." aliandika muitaliano huyo kwenye tweet yake kabla ya kuifuta.
Balotelli amecheza misimu miwili na nusu kwenye klabu ya Manchester City na kuhamia Milan mwezi January mwaka huu - Bolt ni mshabiki mkubwa wa mahasimu wa City klabu ya Manchester United.
0 comments:
Post a Comment