Tuesday, June 18, 2013

BENZEMA, NA RIBERY, NGONO YAWANYIMA AMANI!!!!!

KARIM_BENZEMA13ILE KESI inayowakabili Masupasta Franck Ribery na Karim Benzema ya kufanya ZAHIA_DEHARngono na Changudoa alie chini ya Umri halali leo imeahirishwa baada ya kukwaa kigingi kikubwa cha Sheria ambacho kinaelekea Kesi hiyo itafutwa.
Wanasheria wa Ribery, Miaka 30, na Benzema, Miaka 25, walichachamaa Kortini na kupinga msingi wa Mashitaka hayo kuvunja Haki za kimsingi za Wachezaji hao na Jaji alikubaliana na Wanasheria hao na kuamrisha Mahakama nyingine inayostahili isikilize pingamizi hilo.
Leo Mahakamani, si, Ribery, Benzema wala Zahia Dehar, ambae ndie Binti wanaodaiwa kufanya nae mapenzi kwa malipo, kuwepo.
Ribery na Benzema wanashitakiwa kwa kufanya ngono na Zahia akiwa na Miaka 16 ambao ni Umri mdogo kupita Sheria inavyoruhusu huko Ufaransa kuwa ngono ya kulipia lazima ifanywe na Mwanamke alie juu ya Miaka 18 lakini ngono ya kawaida ni ruksa kufanya na Msichana wa zaidi ya Miaka 15.
BENZEMA_-RIBERYIkiwa watapatikana na hatia, Ribery na Benzema wanaweza kwenda Jela Miaka 3 na kupigwa Faini isiyozidi Euro 45,000.
Kilio cha msingi cha Wanasheria wa Wachezaji hao humo Mahakamani kilikuwa kwamba Sheria haitendi haki kwa vile Wateja wao hawakuwa na njia ya kutambua kwamba Zahia Dehar alikuwa chini ya Miaka 18.
Kesi hiyo sasa itapelekwa Mahakama ya Juu na ikishindikana huko itabidi ipelekwe Mahakama ya Baraza la Katiba la Ufaransa mlolongo ambao unaweza ukachukua hadi Miezi 6.
Hata hivyo, tangu awali Waendesha Mashitaka waliomba Mahakama waifute Kesi hii baada ya kuridhika kuwa Wachezaji hao hawakujua Umri halisi wa Zahia Dehar kitu ambacho hata mwenyewe Binti huyo alithibitisha kuwaficha kina Benzema na Ribery.
Wakati Ribery alikiri kutembea na Zahia Dehar, Benzema amegoma katakata kuwa na uhusiano nae.

0 comments:

Post a Comment