HUKU kukiwa na Mechi 3 zilizobaki kwenye hatua ya Makundi ya kutafuta Nchi 10 zitakazoingia
hatua ya mwisho ya Mtoano ya kupata Nchi 5 zitakazotinga Brazil Mwaka
2014 kwenye Fainali za Kombe la Dunia, Tunisia, Egypt na Congo, Timu
pekee zilizoshinda Mechi zao zote 3 za kwanza, zina nafasi kusonga
Wikiendi hii ikiwa watashinda Mechi zao na matokeo mengine kuwasaidia
huku Nchi yetu, Tanzania, ambayo bado ipo sana kwenye kinyang’anyiro,
ikiwa ugenini kucheza na Morocco.
MUNGU IBARIKI AFRIKA LAKINI PIA IBARIKI TANZANIA!
KUNDI C
Ivory Coast Pointi 7
Tanzania 6
Morocco 2
Gambia 1
Kwenye KUNDI E, Congo wapo Ugenini
kucheza na Gabon na wao, ambao ni Vinara kwa Pointi 6, watafuzu
wakishinda na pia Mechi nyingine kati ya Niger na Burkina Faso
ikimalizika sare.
Nao Egypt, Vinara wa KUNDI G, wataingia
Raundi ya Mwisho wakishinda Mechi yao ya Ugenini na Zimbabwe na wakati
huo huo Mozambique kutoka Sare Ugenini na Guinea.
Tunisia, ambao wako KUNDI B, watafuzu
wakiifunga Sierra Leone Ugenini na wakati huo huo Equatorial Guinea
wakishindwa kuifunga Cape Verde Islands.
Kwenye
KUNDI D, Zambia wanaongoza kwa Pointi 1 mbele ya Ghana, Jumamosi wako
Nyumbani kucheza na Lesotho na Ghana wana Mechi ngumu Ijumaa Usiku
Ugenini huko Khartoum kuivaa Sudan.
Cameroon, chini ya Kocha mpya Volker
Finke, wako Ugenini kucheza na Togo wakisaka kuendeleza uongozi wao
KUNDI I wa Pointi 1 dhidi ya Libya ambao Ijumaa Usiku wako Nyumbani
kucheza na Congo DR, hii ikiwa Mechi yao ya kwanza kucheza Nchini kwao
katika Miaka miwili.
Cameroon watacheza Mechi yao bila ya
Staa wao Samuel Eto'o ambae aliumia akiiwakilisha Klabu yake Anzhi
Makhachkala kwenye Fainali ya Kombe la Russia.
Mechi za Raundi ya 4 ya Hatua ya Makundi
za KUNDI F zilichezwa mapema Jumatano kwa vile Nigeria wanahitajika
kuliwakilisha Bara la Afrika kama Mabingwa wao huko Brazil kwenye Mashindano ya Fifa ya kombe la mabara yanayoanza Juni 15.
RATIBA/MATOKEO:
Jumatano Juni 5
Kenya 0-1 Nigeria
Malawi 0-0 Namibia
Ijumaa Juni 7
18:30 Libya v Congo, DR
20:00 Sudan v Ghana
Jumamosi Juni 8
16:00 Uganda v Liberia
16:00 Zambia v Lesotho
16:00 Botswana v Ethiopia
17:00 Central African Republic v South Africa
17:30 Gabon v Congo
18:00 Angola v Senegal
19:30 Gambia v Ivory Coast
19:30 Sierra Leone v Tunisia
20:30 Cape Verde v Equatorial Guinea
23:00 Morocco v Tanzania
Jumamosi Juni 8
Niger v Burkina Faso
Zimbabwe v Egypt
Guinea v Mozambique
Benin v Algeria
Mali v Rwanda
Togo v Cameroon
RAUNDI YA PILI
[Kila Timu imecheza Mechi 3 isipokuwa inapotajwa]
KUNDI A
Ethiopia Pointi 7
South Africa 5
CAR 3
Botswana 1
KUNDI B
Tunisia Pointi 9
Sierra Leone 4
Eq Guinea 4
Cape Verde 0
KUNDI C
Ivory Coast Pointi 7
Tanzania 6
Morocco 2
Gambia 1
KUNDI D
Zambia Pointi 7
Ghana 6
Lesotho 2
Sudan 1
KUNDI E
Congo Pointi 9
Burkina Faso 3
Niger 3
Gabon 3
KUNDI F
[Kila Timu imecheza Mechi 4]
Nigeria Pointi 8
Malawi 6
Namibia 4
Kenya 2
KUNDI G
Egypt Pointi 9
Guinea 4
Mozambique 2
Zimbabwe 1
KUNDI H
Algeria Pointi 6
Mali 6
Benin 4
Rwanda 1
KUNDI I
Cameroon Pointi 6
Libya 5
Congo DR 4
Togo 1
KUNDI J
Senegal Pointi 5
Liberia 4
Angola 3
Uganda 2
0 comments:
Post a Comment