Wednesday, August 7, 2013

Tazama picha za Mtoto wa Usher Raymond anusurika kufa na mama mzazi afungua mashtaka kudai kurudishiwa watoto wake


Mtoto a Usher Raymond mwenye miaka 5 amewahishwa  hospitali kitengo cha watu mahututi (ICU) baada ya kunusurika kuzama ndani ya pool la kuogelea. Raymond V alikuwa na shangazi yake ndani ya pool lililopo nyumbani pale alipokwama katika tundu la pool hiyo alipokuwa akijaribu kufata toy.
Shangazi huyo na mfanya kazi walishindwa kutoa mkono wa mtoto huyo uliokuwa umenasa katika tundu hilo na kuanza kupiga makelele.
wafanyakazi waliokuwa akishughulikia audio na visual katika nyumba hiyo walikimbia na kujirusha kwenye pool na kumuokoa mtoto huyo ambapo iliwalazimu kumfanyia CPR (kumkandamiza kifuani) na hatimae kufanikiwa kumzindua.
Raymond V aliwahishwa hospitali ambapo anasemekana kuurudi katika hali yake ya ufahamu na anaendelea vizuri, Usher Raymond hakuwepo nyumbani kwake wakati tukio linatokea 
Raymond V ni mdogo wa watoto wawili wa Usher na mkewe wa zamani, Tameka Raymond, na alikabidhiwa na kupewa ruhusa ya kuwaangalia watoto wake  Agosti 2012, baada ya kutalakiana na mkewe huyo.
Mke huyo wa zamani wa Usher amepeleka hati za kisheria kuomba dharura ya kusikilizwa haraka wiki hii katika jitihada za kururudishiwa watoto wake baada ya baba yao kushindwa majukumu yake kama baba na kuwaachia watu wengine kuwaangalia watoto wake.

Ajali ya jana imetokea ikiwa ni mwaka tu tangu mtoto wa kambo wa Usher Kile Glover mwenye miaka 11 kufariki kwa ajali ya Jet Ski akiwa katika ziwa Lanier, Georgia.
 posted by The superonenews.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment