Tuesday, February 4, 2014

MAUAJI WATU 16 MARA: MAPENZI, UCHAWI, VISASI VYATAJWA: soma zaid



Marehemu Juma Marwa Nyaitara.WAKATI hofu kubwa ikiwa imetanda miongoni mwa wananchi wa Wilaya za Butiama na Tarime mkoani Mara kutokana na mauaji ya watu zaidi ya 16, imebainika kwamba sababu za vifo hivyo zimejikita katika wivu wa kimapenzi, vitendo vya ulipizaji visasa na imani za kishirikina.


Kwa mujibu wa taarifa kutoka vyanzo mbalimbali mkoani humo, mauaji hayo, hasa ya akina mama, yamekuwa yakifanyika mchana wakati wakiwa katika shughuli za kilimo, kitu ambacho kimewafanya kuogopa mno na kubadili hata ratiba ya kulala, kwani hivi sasa wanalala mapema zaidi.
Zacharia Chacha Mwita enzi za uhai wake.
“Kule kijijini kwetu hali ni mbaya sana kiasi kwamba akina mama ambao ndiyo waathirika wengi wa mauaji haya, wamekuwa na hofu kubwa kiasi cha kuwafanya wasiende shambani pia wanalala mapema.
“Kwa kipindi cha mwezi mmoja jumla ya watu nane wameuawa, lakini mpaka sasa hakuna aliyekamatwa akihusishwa na matukio hayo, nafikiri jaribu kuwasiliana na mwenyekiti wa kijiji chetu atakupa ukweli zaidi,”alisema Mwita Marwa aliyedai ni mkazi wa Kijiji cha Mtiriri ambaye kwa sasa yupo Dar.
Muuaji anadaiwa kuvaa vazi kama hili la Kininja.
Mwenyekiti wa kijiji hicho, Pascal Maerere alikiri kuwepo kwa mauaji hayo na kuwataja waliouawa kuwa ni pamoja na Nyabuturi Makanga ambaye mwili wake ulikutwa porini Januari 10, mwaka huu ukiwa umechinjwa huku sehemu ukiwa umeliwa na wanyama.
Jeneza lenye mwili wa marehemu David Mwasi Yomami aliyezikwa Nyamwaga.
Wengine waliouawa ni Upendo Manyama aliyevamiwa nyumbani kwake na kukatwa mapanga hadi kufa Desemba 12, mwaka jana. Januari 6, mwaka huu, mwanaume ambaye hakufahamika jina alikutwa shambani akiwa ameuawa.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa msibani kwa marehemu David Mwasi Yomami.
Mkaguru Magee, mwili wake ulikutwa wiki iliyopita ukiwa umefukiwa wakati Juni 8, mwaka jana, mtu moja aliyedaiwa kutoka Musoma mjini aliuawa na mwili wake kukutwa na majeruhi. Polisi waliuchukua mwili huo ambao jina lake halikujulikana.
Samwel Richard Mohenga (37) wa kijiji cha Rebu, Mara enzi za uhai wake.
Ziada John, mkazi wa kijiji jirani cha Nyasurura, mwili wake ulikutwa katika pori ukiwa umenyongwa kwa kutumia nguo yake wakati Nkwaya Busia, mkazi wa kijiji hicho alienda kulima shambani kwake lakini baadaye mwili wake ulikutwa ukiwa na alama ya kuchomwa kisu.
Mwingine aliyejulikana kwa jina la mama Khadija, mkazi wa Musoma mjini naye alikutwa amekufa kijijini hapo kwa kukatwa panga na mwili wake kuokotwa porini Mei 28, mwaka juzi.
Mwenyekiti huyo alisema matukio hayo huenda yanatokana na mambo ya kishirikina, visa vya mapenzi, ujambazi au kisasi.
Marehemu Busia.
“Kwa kweli inauma sana, watu wanachinjwa kama kuku, wanapigwa risasi hadharani,” alisema kiongozi huyo.
Katika Wilaya ya Tarime, wananchi nane nao wameuawa na mtu mmoja anayejifunika uso kama ninja anayetumia bunduki aina ya SMG ambaye hadi sasa hajaweza kupatikana.
Waliotajwa kuuawa kwa risasi na mtu huyo anayehisiwa kutaka kulipiza kisasi na ambaye anaripotiwa kuvaa Kininja ili kuficha sura ni Juma Mwita Mtodi (68), Chacha Robert Kisiri (36), Chacha Marwa (58), Erick Lucas Mohabe (24), Juma Mwita Nyaitara, David Yomani, Samwel Richard na Sami Magori mwenye umri wa miaka 35.
Marehemu Upendo enzi za uhai wake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Frednand Mtui alikiri kupitia simu yake ya mkononi kutokea kwa mauaji hayo na ili kupata dawa, ameshakutana na viongozi wa dini, wananchi ili kuimarisha ulinzi kwa kila mtaa.
“Unajua haya mauaji mara nyingi hutokea mchana, hasa kwa akina mama na inawezekana mambo ya kishirikina yakawa yametawala, nimewaagiza kutoenda shambani mtu mmoja mmoja na vijana wangu wanaendelea na uchunguzi wa kina,” alisema Kamanda Mtui. posted by http://thesuperonenews.blogspot.com/

0 comments:

Post a Comment