Thursday, January 9, 2014

MISS’ AANGUKA, AZIMIA AKOMBWA KILA KITU



Ama kweli dunia haina huruma! Dada Happy amejikuta akiishiwa nguvu na kuanguka mbele ya kadamnasi na kuzimia pasipo msaada wowote ambapo badala yake watu waliodaiwa kuwa ni vibaka walimuibia vitu vyake vyote.

Kwa mujibu wa mashuhuda, mrembo huyo ambaye alikuwa katika mishemishe za kawaida alidondoka ghafla akiwa Mitaa ya Nyakato jijini hapa mbele ya kituo cha polisi, Januari 4, mwaka huu.
Ilidaiwa  kuwa baada ya kupoteza fahamu, wahuni walimliza simu pamoja na fedha zote kisha kumwacha akiwa hana msaada wowote.
Hata hivyo, dada huyo alisaidiwa na wasamaria wema ambao walimpeleka Hospitali ya Buzuruga ambapo alipatiwa matibabu na baadaye ndugu zake walipata taarifa kutoka kwa mashuhuda wanaomjua Happy kisha wakaenda kumchukua.
Gazeti hili lilitaka kujua kilichompata mrembo huyo lakini madaktari hospitalini hapo walidai hawawezi kutoa siri ya mgonjwa huku ndugu nao wakiweka ngumu kusema kilichosababisha Happy kudondoka ghafla na kupoteza fahamu.
“Mimi sijui kilichompata lakini sasa hivi hali ni mbaya. Unaweza ukashangaa mtu kasimama halafu akadondoka ghafla na kupoteza maisha. Cha msingi tucheki afya zetu mara kwa mara,” alisema mmoja wa ndugu hao ambaye hakutaka kutajwa gazetini.

0 comments:

Post a Comment