Thursday, January 9, 2014

BORA KWA DESEMBA: DAVID MOYES ATEULIWA KUGOMBEA MENEJA BORA!


MOYES-NGUMI_JUU

WAGOMBEA MCHEZAJI BORA NI 6!!
BOSI wa Manchester United David Moyes ni miongoni mwa Mameneja kadhaa Wanaogombea Tuzo ya Meneja Bora ya Barclays ya Ligi Kuu England, 
Tuzo ambayo hutolewa na Wadhamini.
Wadhamini wa Ligi Kuu England, ni Kampuni ya Barclays, ambayo hutumia Jopo maalum kuteua Wagombea.
Mwezi Desemba, Man United ilicheza Mechi 7 za Ligi na Kushinda 4, Sare 1 na Kufungwa 2.
Wagombea wengine ni Meneja wa Man City, Manuel Pellegrini, ambae hakufungwa hata Mechi moja na pia wamo Jose Mourinho wa Chelsea na yule wa Everton, Roberto Martinez.
++++++++++++++++++++++++
MAN UNITED=Mwezi Desemba
-1 Desemba v Tottenham (Ugenini) Sare 2-2
-4 Desemba v Everton (Nyumbani) Kipigo 1-0
-7 Desemba v Newcastle (Nyumbani) Kipigo 1-0
-15 Desemba v Aston Villa (Ugenini) Ushindi 3-0
-21 Desemba v West Ham (Nyumbani) Ushindi 3-1
-26 Desemba v Hull (Ugenini) Ushindi 3-2
-28 Desemba v Norwich (Ugenini) Ushindi 1-0
++++++++++++++++++++++++
Kwa upande wa Wachezaji, Wagombea wa Mchezaji Bora kwa Mwezi Desemba wapo 6 na miongoni mwao ni Straika wa Liverpool, Luis Suarez, ambae amefunga Bao 20 katika Mechi 15 za Ligi.
Wengine ni Wachezaji watatu wa Man City, Alvaro Negredo, Vincent Kompany na Yaya Toure.
Pia wamo Ross Barkley wa Everton na Straika wa Arsenal Theo Walcott ambae Wiki hii amepata pigo kubwa baada kuumia Goti litakalomweka nje ya Uwanja kwa Miezi 6 ikimaanisha kuwa hatacheza Mechi yeyote tena Msimu huu na pia kutoichezea England kwenye Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil Mwezi Juni.
RATIBA:
Jumamosi Januari 11
[Saa za Bongo]
1545 Hull v Chelsea
1800 Cardiff v West Ham
1800 Everton v Norwich
1800 Fulham v Sunderland
1800 Southampton v West Brom
1800 Tottenham v Crystal Palace
2030 Man Utd v Swansea
Jumapili Januari 12
1705 Newcastle V Man City
1910 Stoke V Liverpool
Jumatatu Januari 13
MSIMAMO:
NA TIMU P GD PTS
1 Arsenal 20 21 45
2 Man City 20 34 44
3 Chelsea 20 19 43
4 Liverpool 20 23 39
5 Everton 20 13 38
6 Tottenham 20 -1 37
7 Man Utd 20 9 34
8 Newcastle 20 4 33
9 Southampton 20 3 27
10 Hull 20 -3 23
11 Aston Villa 20 -6 23
12 Stoke 20 -11 22
13 Swansea 20 -2 21
14 West Brom 20 -4 21
15 Norwich 20 -16 20
16 Fulham 20 -21 19
17 Cardiff 20 -17 18
18 Crystal Palace 20 -16 17
19 West Ham 20 -11 15
20 Sunderland 20 -18 14

0 comments:

Post a Comment