MWANDISHI
wa habari wa ITV na Radio One, Ufoo Saro (pichani) amepigwa risasi ya
tumbo na kujeruhiwa vibaya, huku mama yake mzazi akipoteza maisha baada
ya kupigwa risasi katika tukio hilo leo alfajiri............................................................................
Mwandishi huyo pamoja na mama yake wamefanyiwa kitendo hicho na
kijana anayedaiwa kuwa ni mpenzi wa Ufoo Saro, aitwaye Mushi ambaye
inadaiwa alikuwa nao katika mazungumzo eneo la Kibamba nje kidogo ya
jiji la Dar es Salaam ambapo aliwapiga risasi na yeye kujiua kwa risasi.
Mtuhumiwa aliyefanya kitendo hicho anadaiwa kuwa mfanyakazi wa shirika moja la UN.
0 comments:
Post a Comment