Tuesday, October 15, 2013

Je wajua Watoto milioni mbili na nusu hawako shuleni Tanzania?

   



Sababu zinazowakimbiza wanafunzi shuleni ziko nyingi, ikiwamo shule nyingi kuwa na mazingira yasiyokuwa rafiki kwa wanafunzi kama inavyoonekana kwenye picha hii ambapo somo linaendelea chini ya mti badala ya darasani. 

Anataja sababu nyingine kuwa ni  mimba za utotoni, ambazo hata hivyo anasema zinachangia sehemu ndogo ya watoto kutokuwa shuleni.



Tafiti zinaonyesha sababu za wanafunzi kutokuwapo shuleni ni pamoja na utoro, mimba za utotoni, umaskini na mwamko mdogo wa wazazi kuhusu elimu.
Wakati ripoti ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 , ikionyesha kuwa asilimia 44 ya Watanzania wote ni watoto chini ya umri  wa miaka 15, watoto milioni mbili na nusu  wamebainika kukosa fursa ya kupata elimu ya msingi.
Msemaji wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Ntambi Bunyazu, anasema kuwa sababu kubwa ya watoto wengi kutokuwapo shuleni licha ya kuwa na umri wa kwenda shule  ni utoro.
“Hata ukiangalia BEST (Kitabu cha Takwimu za Elimu ya Msingi) ya mwaka 2012 utaona kuwa utoro ulikuwa sababu kubwa ya watoto kutokuwa shuleni,” anasema.
Anaeleza kuwa, utoro huo unachangiwa na mambo kadhaa, ikiwamo umaskini na baadhi ya wazazi kutokuona umuhimu wa elimu.
Anataja sababu nyingine kuwa ni  mimba za utotoni, ambazo hata hivyo anasema zinachangia sehemu ndogo ya watoto kutokuwa shuleni.
Kuhusu watoto wasioandikishwa kabisa shuleni, Bunyazu anasema kuwa hali hiyo inachangiwa na wazazi kutokuona umuhimu wa elimu kwa watoto wao.
Tatizo la dunia
Siyo Tanzania pekee, tatizo la watoto kukosa fursa za elimu linaikabili dunia nzima. Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki –Moon, hadi kufikia mwaka 2011, takwimu zinaonyesha watoto milioni 57 hawakuwepo shuleni.
“Watoto milioni 57 hawako shuleni, wanarandaranda mitaani. Kila ninapotembelea nchi kama vile huko Afrika nimeona watoto wanarandaranda mitaani au wanacheza, kwa nini wako hapo?’’ anahoji na kuongeza:
 “Wanapaswa wakati huo wawepo shuleni. Hiyo ni dira yetu, lazima wote tuwarudishe shule. Kila siku watoto 19,000 wenye umri chini  ya miaka mitano wanakufa kutokana na magonjwa yanayozuilika. Ni lazima tuokoe vifo hivyo vinavyoweza kuepukika.”
Akizungumza katika maadhimisho ya miaka 50 ya Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Weruweru, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alikiri kuwepo kwa changamoto nyingi katika sekta mbalimbali ikiwamo elimu.Posted by thesuperonenews.blogspot.com

0 comments:

Post a Comment