Tottenham wametoka Sare Bao 1-1 na Chelsea na kuipiku Arsenal kileleni mwa Ligi Kuu England
Gylfi Sigurdsson ndie alieifungia Spurs
Bao katika Kipindi cha Kwanza baada ya ushirikiano mzuri kati ya
Christian Eriksen na Roberto Soldado na Mpira kumfikia yeye.
MAGOLI:
Tottenham 1
Sigurdsson Dakika ya 19
Chelsea 1
Terry Dakika ya 65
Chelsea walimwingiza Juan Mata mara
Kipindi cha Pili kilipoanza na frikiki yake ndio iliunganishwa na John
Terry kwa kichwa na kusawazisha Bao.
MSIMAMO:
NA |
TIMU |
MECHI |
PTS |
1 |
Tottenham |
6 |
13 |
2 |
Arsenal |
5 |
12 |
3 |
Chelsea |
6 |
11 |
4 |
Man. City |
5 |
10 |
5 |
Liverpool |
5 |
10 |
6 |
Everton |
5 |
9 |
Chelsea walimaliza Mechi wakiwa Mtu 10
baada ya Fernando Torres kupewa Kadi ya Njano ya pili na kutolewa nje
kwa Kadi Nyekundu zikiwa zimebaki Dakika 10 Mpira kwisha.
Sare hii imewafanya Chelsea wakamate Nafasi ya 3.
Kivutio cha Mechi hii kilikuwa mzozo
kati ya Andre Villas-Boas na Jose Mourinho, Watu ambao wanatoka Nchi
moja Ureno na walifanya kazi pamoja kwa Miaka 7, waliporushiana maneno
lakini kabla ya Mechi kuanza walipeana mikono na mwisho wa Mechi
kukumbatiana.
VIKOSI:
Spurs: Lloris, Walker, Dawson, Vertonghen, Naughton, Paulinho, Dembele, Townsend, Eriksen, Sigurdsson, Soldado
Akiba: Chiriches, Lamela, Holtby, Defoe, Chadli, Friedel, Sandro.
Chelsea: Cech, Ivanovic, Luiz, Terry, Cole, Ramires, Mikel, Lampard, Oscar, Torres, Hazard
Akiba: Essien, Mata, Schurrle, Schwarzer, Cahill, Azpilicueta, Eto'o.
Refa: Mike Dean
RATIBA:
BPL: LIGI KUU ENGLAND
Jumapili 29 Septemba
15:30 Stoke City v Norwich City
18:00 Sunderland v Liverpool
Jumatatu 30 Septemba
22:00 Everton v Newcastle United
Posted by Thesuperonews.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment