Sunday, September 29, 2013

EL DERBI MADRILEÑO: REAL WAKIONA CHA MOTO, NI MARA YA KWANZA TANGU 99!

EL_DERBI_MADRILENO13
Real Madrid wamepoteza El Derbi Madrileno baada ya kuchwapwa kwao Santiago Bernabeu Bao 1-0 na Atletico Madrid ambao Jana walimaliza ile Rekodi ya kutoifunga Real kwenye La Liga tangu Mwaka 1999 zikiwa ni Mechi 23.

NI DIEGO COSTA SHUJAA WA ATLETICO!!
BUNDESLIGA: DORTMUND YAFUMUA 5, BAYERN 1 TU!!
SERIE A: NAPOLI, AC MILAN ZASHINDA!
Bao la ushindi kwa Atletico lilifungwa na Mbrazil Diego Costa katika Dakika ya 11.
Ushindi huo umewafanya Atletico wabaki kileleni wakifungana kwa Pointi na Barcelona, ambao Jana waliifunga Almeria Bao 2-0, na wote sasa wana Pointi 21 kila mmoja baada Mechi 7 lakini Barca wako juu kwa ubora wa Magoli.
Real wamebaki Nafasi ya 3 wakiwa Pointi 5 nyuma.
Katika Mechi ya Barca na Almeria, Lionel Messi aliifungia Barca Bao la kwanza lakini akalazimika kutoka baada ya kupata matatizo ya Musuli.
Bao la Pili la Barca lilifungwa na Adriano.
Huko Germany kwenye Bundesliga, Vinara Borussia Dortmund waliinyuka Freiburg Bao 5-0 na Mabingwa Watetezi Bayern Munich kuifunga VfL Wolfsburg 1-0.
Bao za Dortmund zilifungwa na Marco Reus na Robert Lewandowski, Bao 2 kila mmoja na Jakub Blaszczykowski kupiga Bao la tano.
Kwenye Mechi ya Bayern Munich, Thomas Muller ndie aliefunga Bao pekee.
Matokeo hayo yanaifanya Dortmund ikamate usukani ikiwa na Pointi 19 sawa na Bayern Munich ambao wako Nafasi ya Pili kwa kuzidiwa ubora wa magoli.
Huko Italy kwenye Serie A. AC Milan na Napoli zote zilishinda kwa AC Milan kuipiga 1-0 Sampdoria kwa Bao la Birsa na Napoli kuichapa Genoa 2-0 Bao zote zikifungwa na Pandev.
RATIBA/MATOKEO
Jumamosi Septemba 28
Valencia 1 Rayo Vallecano 0
UD Almeria 0 FC Barcelona 2
Real Sociedad 1 Sevilla FC 1
Real Madrid CF 0 Atletico de Madrid 1
Jumapili Septemba 29
13:00 Osasuna v Levante
18:00 Celta de Vigo v Elche CF
20:00 RCD Espanyol v Getafe CF
22:00 Real Betis v Villarreal CF
Jumatatu Septemba 30
23:00 Granada CF v Athletic de Bilbao
SERIE A
Jumamosi Septemba 28
Genoa 0 Napoli 2
AC Milan 1 Sampdoria 0
Jumapili Septemba 29
13:30 Torino FC v Juventus
16:00 Atalanta v Udinese
16:00 Hellas Verona v Livorno
16:00 Sassuolo v SS Lazio
21:45 AS Roma v Bologna
Jumatatu Septemba 30
21:45 Fiorentina v Parma
BUNDESLIGA
Jumamosi Septemba 28
Bayer 04 Leverkusen 2 Hannover 0
Bayern Munich 1 VfL Wolfsburg 0
BV Borussia Dortmund 5 SC Freiburg 0
Hertha Berlin 3 FSV Mainz 1
TSG Hoffenheim 3 Schalke 3
Eintracht Frankfurt 2 Hamburger SV 2
Jumapili Septemba 29
16:30 SV Werder Bremen v FC Nuremberg
18:30 Eintr. Braunschweig v VfB Stuttgart 

0 comments:

Post a Comment