Saturday, September 14, 2013

LIGI KUU ENGLAND: ARSENAL MTEREMKO3, SPURS 2, CITY SARE!!


BPL2013LOGO
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA/MATOKEO:
Jumamosi 14 Septemba
Man United 2 Crystal Palace 0
Aston Villa 1 Newcastle United 2
Fulham 1 West Bromwich Albion 1
Hull City 1 Cardiff City 1
Stoke City 0 Manchester City 0
Sunderland 1 Arsenal 3
Tottenham Hotspur 2 Norwich City 0
19:30 Everton v Chelsea

STOKE 0 MAN CITY 0
Stoke City na Man City zilitoka sare ya Bao 0-0 kwenye Mechi ambayo Stoke walionekana kuja juu sana.
VIKOSI:
Stoke: Begovic, Cameron, Shawcross, Huth, Pieters, Walters, Nzonzi, Adam, Wilson, Etherington, Jones
Akiba: Whelan, Pennant, Palacios, Arnautovic, Crouch, Sorensen, Ireland.
Man City: Hart, Zabaleta, Javi Garcia, Nastasic, Kolarov, Toure, Rodwell, Milner, Jovetic, Nasri, Negredo
Akiba: Lescott, Dzeko, Jesus Navas, Aguero, Fernandinho, Pantilimon, Boyata.
Refa: Mark Clattenburg
ASTON VILLA 1 NEWCASTLE 2
Bao za Hatem Ben Arfa na Yoan Gouffran  leo zimewapa Newcastle ushindi wa Ugenini wa Bao 2-1 walipocheza na Asyon Villa ambao Bao lao moja  lilifungwa na Christian Benteke .
VIKOSI:
Aston Villa: Guzan, Lowton, Vlaar, Okore, Luna, El Ahmadi, Westwood, Agbonlahor, Delph, Benteke, Weimann
Akiba: Steer, Clark, Bacuna, Helenius, Sylla, Tonev, Kozak.
Newcastle: Krul, Debuchy, Coloccini (c), Yanga-Mbiwa, Santon; Anita, Sissoko, Cabaye; Remy, Cisse, Ben Arfa.
Akiba: Elliot, Dummett, S.Taylor, Tiote, Marveaux, Sammy Ameobi, Gouffran.
Refa: Mike Dean
HULL CITY 1 CARDIFF 1
Curtis Davies aliwapa Hull City Bao la kuongoza na Cardiff City kusawazisha kwa Bao la Peter Whittingham na Mechi hii kwisha Bao 1-1.
VIKOSI:
Hull: McGregor, Elmohamady, Chester, Davies, Figueroa, Koren, Huddlestone, Livermore, Brady, Aluko, Graham
Akiba: Rosenior, Bruce, Meyler, McShane, Jakupovic, Boyd, Quinn.
Cardiff: Lewis, Theophile-Catherine, Turner, Caulker, Taylor, Kim, Cowie, Gunnarsson, Medel, Whittingham, Campbell
Akiba: Hudson, Odemwingie, Gestede, Noone, Mutch, Maynard, Moore.
Refa: Robert Madley
SUNDERLAND 1 ARSENAL 3
Aaron Ramsey aliifungia Arsenal Bao 2 walipoitandika Sunderland Bao 3-1 huko Stadium of Light.
Mchezaji mpya wa Arsenal, Mesut Ozil, ambae alicheza vizuri, ndie aliempa pasi Olivier Giroud kufunga Bao la Dakika ya 11 lakini Sunderland walisawazisha kwa Bao la Penati ya Craig Gardner katika Kipindi cha Pili.
Lakini baada ya Ramsey kufunga Bao la Pili kwa Arsenal, Refa Martin Atkinson alileta utata mkubwa pale Jozy Altidore alipomtoka Bacary Sagna na kufunga Bao lakini Refa huyo aliashiria kuwa Sagna alicheza Faulo kabla Bao kufungwa na kuwaacha Sunderland wakilalamika kwanini Bao halikubaki.
Hata hivyo, Ramsey akafunga Bao la 3 na kuwanyamazisha Sunderland na kuipa Arsenal ushindi wa Bao 3-1.
VIKOSI:
Sunderland: Westwood, Celustka, Diakite, Roberge, Colback, Johnson, Ki, Vaughan, Mavrias, Altidore, Fletcher
Akiba: Brown, Larsson, Gardner, Wickham, Cuellar, Mannone, Borini.
Arsenal: Szczesny, Jenkinson, Sagna, Koscielny, Gibbs, Wilshere, Flamini, Ozil, Walcott, Giroud, Ramsey
Akiba: Vermaelen, Monreal, Fabianski, Frimpong, Miyaichi, Gnabry, Akpom.
Refa: Martin Atkinson
TOTTENHAM 2 NORWICH 0
Bao mbili za Gylfi Sigurdssonleo zimewapa ushindi wa Bao 2-0 Totenham walipoifunga Norwich City na pia kumchezesha Mchezaji wao mpya Christian Eriksen ambae alitengeneza Bao la kwanza.
VIKOSI:
Spurs: Lloris, Walker, Dawson, Vertonghen, Rose, Dembele, Paulinho, Townsend, Eriksen, Sigurdsson, Soldado
Akiba: Kaboul, Holtby, Naughton, Defoe, Friedel, Sandro, Lamela.
Norwich: Ruddy, Whittaker, Turner, Bassong, Garrido, Snodgrass, Fer, Johnson, Redmond, Elmander, van Wolfswinkel
Akiba: Martin, Howson, Hooper, Pilkington, Bunn, Olsson, Tettey.
Refa: Lee Mason
FULHAM 1 WEST BROM 1
Bao la Dakika ya 90 la Gareth McAuley kwa Kichwa kufuatia Kona ya Chris Brunt  limewaokoa West Brom na kupata Sare ya Bao 1-1 huko Craven Cottage walipocheza na Fulham.
Kiungo wa Fulham, Steve Sidwell, ndie aliewafungia Fulham Bao lao katika Dakika ya 22.
VIKOSI:
Fulham: Stockdale, Riether, Senderos, Hangeland, Richardson, Ruiz, Sidwell, Parker, Kacaniklic, Kasami, Berbatov
Akiba: Karagounis, Duff, Taarabt, Rodallega, Zverotic, Amorebieta, Etheridge.
West Brom: Myhill, Billy Jones, McAuley, Olsson, Ridgewell, Amalfitano, Mulumbu, Yacob, Brunt, Anelka, Anichebe
Akiba: Popov, Morrison, Rosenberg, Sinclair, Luke Daniels, Dawson, Berahino.
Refa: Lee Probert
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
Jumapili 15 Septemba
18:00 Southampton v West Ham United
Jumatatu 16 Septemba
22:00 Swansea City v Liverpool

0 comments:

Post a Comment