BAADHI
ya Klabu za Ligi Kuu England, zikiwemo Mabingwa Manchester United,
Tottenham na Norwich City, zimegoma kutoa sapoti kwenye Kampeni ya
Kutetea Haki za Ushoga.
KLABU 29 ZINAZOSAPOTI MASHOGA:
-LIGI KUU ENGLAND: Arsenal, Aston Villa, Crystal Palace, Liverpool, Manchester City, Norwich, Sunderland, West Ham, West Brom
-CHAMPIONSHIP: Birmingham, Blackburn, Doncaster, Huddersfield, Ipswich, Leicester, Millwall, Sheffield Wednesday
-LIGI 1: Carlisle, Crewe, Gillingham, Leyton Orient, MK Dons, Peterborough, Preston, Tranmere
-LIGI 2: Bristol Rovers, Exeter, Dagenham & Redbridge, Northampton
**LISTI IMEHAKIKIWA TAREHE 18 Machi 2013
Hivi
Majuzi, Wachezaji wa Soka huko England na Scotland walialikwa kuisaidia
Kampeni ya kuunga mkono Mashoga kwa kutakiwa kufunga Nyuzi za Rangi ya
‘Upinde wa Mvua’ kwenye Buti zai wakati wa Mechi za Wikiendi hii na
Taasisi ya Hisani ya Mashoga, Stonewall, ilishamsambaza Nyuzi hizo
spesho kwa Vilabu 92 vya Ligi Kuu England na Klabu za Ligi za Madaraja
ya chini na pia Klabu 42 za Soka ya Kulipwa huko Scotland.
Kwenye Kampeni hii, iitwayo The Right
Behind Gay Footballers, Wachezaji wameombwa kutumia Nyuzi hizo kwenye
Mechi za Septemba 21 na 22.
Lakini Klabu nyingi zimeonyesha
kutoridhishwa kwao kwa jinsi Kampeni hiyo inavyoendeshwa na Taasisi ya
Hisani ya Mashoga, Stonewall, na Kampuni ya Kamari, Paddy Powers, bila
ya wao kuhusishwa tangu awali.
Tamko rasmi la Mabingwa Manchester
United limesema Klabu hiyo haitavaa Nyuzi hizo huku nao Tottenham wakiwa
na msimamo huo huo pamoja na Norwich ambao Meneja wao Chris Hughton
amesema Wachezaji wake hawatavaa Nyuzi hizo.
Juzi Wasimamizi wa Ligi Kuu England walisema ni juu ya Klabu na Wachezaji kuamua msimamo wao juu ya Kampeni hii.
HABARI ZA AWALI:
LIGI KUU ENGLAND: NI JUU YA KLABU, WACHEZAJI KUAMUA KUVAA NYUZI ZA ‘USHOGA’!!
Wednesday, 18 September 2013 16:35
>>WIKIENDI WACHEZAJI KUVAA BUTI ZENYE NYUZI RANGI ‘UPINDE WA MVUA!’
WASIMAMIZI wa LIGI KUU ENGLAND wamesema
ni juu ya Klabu zenyewe na Wachezaji wenyewe kuamua kama wataunga mkono
Kampeni ya Kutetea Haki za Mashoga kwa kufunga Nyuzi za Rangi ya ‘Upinde
wa Mvua’ kwenye Buti zao wakati wa Mechi za Ligi za Wikiendi hii.
Tayari Taasisi ya Hisani ya Mashoga,
Stonewall, imetuma Nyuzi hizo spesho kwa Vilabu 92 vya Ligi Kuu England
na Klabu za Ligi za Madaraja ya chini na pia Klabu 42 za Soka ya Kulipwa
huko Scotland.
Kwenye Kampeni hii, iitwayo The Right
Behind Gay Footballers, Wachezaji wataombwa kutumia Nyuzi hizo kwenye
Mechi za Septemba 21 na 22.
Lakini Msemaji wa Ligi Kuu England
amesema: “Ujumbe wa msingi wa Kampeni hii ni mzuri na ni kweli sisi na
Wadau wetu tumeshirikiana na Serikali kuhakikisha Ajenda yote ya Usawa
inaeleweka na tunashiriki. Lakini hatukuhusishwa mapema kwenye Kampeni
hii. Hivyo ni juu ya Klabu na Wachezaji wenyewe kuamua kama
wanaisapoti.”
+++++++++++++++++++++++
HABARI YA AWALI:
WACHEZAJI ENGLAND, SCOTLAND WAALIKWA KUSAIDIA MASHOGA!!
Monday, 16 September 2013 16:27
>>WIKIENDI WAOMBWA KUVAA BUTI ZENYE NYUZI RANGI ‘UPINDE WA MVUA!’
>>ZIJUE KLABU 29 ZINAZOSAPOTI MASHOGA HUKO ENGLAND!!
WACHEZAJI Soka huko England na Scotland
wamealikwa kuisaidia Kampeni ya kuunga mkono Mashoga kwa kutakiwa
kufunga Nyuzi za Rangi ya ‘Upinde wa Mvua’ kwenye Buti zai wakati wa
Mechi za Wikiendi hii inayokuja.
Tayari Taasisi ya Hisani ya Mashoga,
Stonewall, imetuma Nyuzi hizo spesho kwa Vilabu 92 vya Ligi Kuu England
na Klabu za Ligi za Madaraja ya chini na pia Klabu 42 za Soka ya Kulipwa
huko Scotland.
Kwenye Kampeni hii, iitwayo The Right
Behind Gay Footballers, Wachezaji wataombwa kutumia Nyuzi hizo kwenye
Mechi za Septemba 21 na 22.
KLABU 29 ZINAZOSAPOTI MASHOGA:
-LIGI KUU ENGLAND: Arsenal, Aston Villa, Crystal Palace, Liverpool, Manchester City, Norwich, Sunderland, West Ham, West Brom
-CHAMPIONSHIP: Birmingham, Blackburn, Doncaster, Huddersfield, Ipswich, Leicester, Millwall, Sheffield Wednesday
-LIGI 1: Carlisle, Crewe, Gillingham, Leyton Orient, MK Dons, Peterborough, Preston, Tranmere
-LIGI 2: Bristol Rovers, Exeter, Dagenham & Redbridge, Northampton
**LISTI IMEHAKIKIWA TAREHE 18 Machi 2013
Huko Uingereza, haki za Mashoga zinalindwa na hata FA ina msimamo wa kukemea Mashoga kubaguliwa.
Kwa sasa hakuna hata Mchezaji mmoja huko Uingereza alieibuka bayana na kukiri yeye ni Shoga.
Mwaka 1990, Mchezaji wa zamani wa Timu
ya Taifa ya England ya U-21 pamoja, Justin Fashanu, alikuwa ni Mchezaji
wa kwanza wa Kulipwa kutangaza yeye ni Shoga lakini Mwaka 1998, Fashanu
alijiua mwenyewe akiwa na Miaka 37.
0 comments:
Post a Comment