Madrid tayari wamekuwa katika hali ngumukwa kumruhusu Ozil kuondoka kwa ada ya uhamisho ambayo walilipa kwa Bale - hivyo kumfanya mchezaji huyo wa Wales kuwa mchezaji ghali zaidi duniani kwa ada ya uhamisho wa £86million.
Presha kubwa sasa ipo kwa Bale kuelekea mchezo wake wa kwanza na Real Madrid wikiendi ijayo, huku sasa namba za mauzo ya jezi zikionyesha kwamba ni mchezaji aliyembadili ndani ya kikosi cha Carlo Ancelotti ambaye ameshika usukani kwa kuuza jezi nyingi.
Mkurugenzi wa UKSoccershop.com Simon Pretswell alisema: 'Ukiachana na masuala ya uwanjani, sehemu kubwa ya uhamisho ghali duniani huwa umetaliwa na sababu za kibiashara zinazokuja na ukubwa wa mchezaji husika.'
'Katika kesi ya Cristiano Ronaldo, Lionel Messi na mastaa wengine wa zamani kama David Beckham, hawa walileta fedha nyingi kwa klabu kwa mauzo ya jezi kupanda kwa kiasi kikubwa.'
Gareth Bale ameshindwa kuleta mauzo makubwa ya jezi kama ilivyo kwa Mesut Ozil na Neymar walipohamia kwenye vilabu vyao vipya katika dirisha hili la usajili.'
'Kipaji cha Bale hakina mashaka, lakini hajawahi kuwa mmoja ya wauzaji wakubwa wa jezi katika premier league, huku mashabiki wakivutiwa zaidi na jezi za Wayne Rooney, Robin van Persie, Steven Gerrard na even Fernando Torres.
'Posted by thesuperonenen.blogspot.comews
0 comments:
Post a Comment