ALIEWAHI
kuwa Kocha wa Yanga, Tom Saintfiet, ameacha kuwa Kocha wa Timu ya Taifa
ya Malawi mara baada ya kuchapwa Bao 2-0 na Nigeria huko Calabar na
kutupwa nja ya Kombe la Dunia KWENYE Mechi iliyochezwa Jumamosi.
Saintfiet alithibitishwa kuwa Kocha wa
Malawi hapo Julai 2 na Chama cha Soka cha Malawi, FAM, na mwenyewe
ameeleza kuwa alikuwa na makubaliano ya kuwa Kocha hadi Jumamosi Usiku
baada ya Mechi hiyo na Nigeria.
Pia Kocha huyo kutoka Belgium alifafanua
kuwa jukumu lake kubwa lilikuwa ni kuibwaga Nigeria ili wasonge mbele
kwenye Kombe la Dunia lengo ambalo ameshindwa kulitimiza.
Amesema: “Sikuwa hapa kushinda Gemu nyingi! Nilikuwa hapa kushinda Gemu moja tu na Nigeria na hilo ni lengo pekee!”
Mbelgiji huyo alisema hana presha kwa vile makubaliano yake ni mwisho Jumamosi na kuanzia Jumapili ni Mtu huru.
WASIFU:
JINA: Tom Saintfiet
KUZALIWA: 29 Machi 1973 (Miaka 40) MAHALI: Mol, Belgium
KLABU ALIZOCHEZA:
K.V.C. Westerlo
K.F.C. Lommel S.K.
K.F.C. Verbroedering Geel
UMENEJA:
1997-2001 Madaraja ya chini huko Belgium
2000 F.C. Satelitte Abidjan
2002-2003 B71 Sandur
2002-2003 Stormvogels Telstar
2003-2004 Al-Gharafa Sports Club
2004 Qatar U-17
2005-2006 BV Cloppenburg
2006-2007 FC Emmen (Mkurugenzi wa Ufundi)
2008 RoPS
2008-2010 Namibia
2010 Zimbabwe
2010-2011 Shabab Al-Ordon
2011 Ethiopia
2012 Nigeria (Mkurugenzi wa Ufundi)
2012 Yanga
2012-2013 Yemen
2013 Malawi
Saintfiet alicheza Soka kati ya Miaka ya
1983 na 1997 na baadae kuwa Meneja wa Klabu akiwa na Miaka 24 tu na
kuweka historia ya kuwa Meneja mdogo kabisa katika Soka la Belgium.
Hapo Julai 2012, Saintfiet aliteuliwa
kuwa Kocha wa Mabingwa wa Tanzania Bara Yanga na mara tu baada ya uteuzi
huo aliwaongoza kutwaa Ubingwa wa Kagame Cup, Kombe la Klabu Bingwa
Afrika Mashariki na ya Kati, lakini Mwezi Septemba akaondolewa kama
Kocha.
0 comments:
Post a Comment