JUMANNE na Jumatano Usiku zipo Mechi 10 za kwanza za Raundi ya Mchujo ya UEFA CHAMPIONZ LIGI
ambapo Washindi 10 wa Raundi hii watajumuika na Timu 22 ambazo
zimepitishwa moja kwa moja kwenye Droo ya kupanga Makundi na Arsenal ni
moja ya Timu inazosaka kuwemo kwenye hizo 10 lakini ni lazima kwanza
wawatoe Fenerbahce ya Uturuki
.
ALHAMISI: USIKU WA EUROPA LIGI!!
PATA RATIBA na DONDOO MUHIMU YA MECHI HIZO 10:
RATIBA
UEFA CHAMPIONZ LIGI
RAUNDI YA MCHUJO:
[SAA za BONGO]
Jumanne Agosti 20
1800 Shakhter Karagandy v Celtic
2145 Lyon v Real Sociedad
2145 Pacos de Ferreira v Zenit St Petersburg
2145 Viktoria Plzen v NK Maribor
2145 PSV Eindhoven v AC Milan
Jumatano Agosti 21
[Saa 2145]
Fenerbahce v Arsenal
Schalke v PAOK Salonika
Steaua Bucharest v Legia Warsaw
Ludogorets Razgrad v FC Basel
Dinamo Zagreb v Austria Wien
[Marudiano Agosi 27 na 28]
***FAHAMU: Washindi 10 wa hii Raundi ya Mchujo wataingia Hatua ya Makundi ambapo watajumuika na Timu 22 zinazoingia moja kwa moja.
JUMANNE
FC Shakhter Karagandy v Celtic FC
-Hii ni mara ya kwanza kwa Klabu hizi mbili kukutana.
-Kazakhstan ni Nchi ya 36 kwa Celtic
kutembelea katika Mechi za Ulaya lakini kwa Shakhter Karagandy ni mara
ya pili kucheza Ulaya, mara ya kwanza ikiwa kwenye UEFA Intertoto Cup
Mwaka 2006.
Olympique Lyonnais v Real Sociedad de Fútbol
-Real Sociedad hawajacheza Ulaya tangu wafungwe 2-0 na Lyon kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu wa 2003/04.
FC Paços de Ferreira v FC Zenit St Petersburg
-Zenit hawajawahi kushinda Portugal na
wameshafungwa mara mbili na Timu za huko walipochapwa Jumla ya Bao 5-4
na CD Nacional 2009/10 kwenye UEFA Europa Ligi na Jumla ya 4-3 na SL
Benfica 2011/12 kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI.
-Paços walianza kucheza Ulaya 2007/08 kwenye UEFA Cup na kufungwa Jumla ya 1-0 katika Mechi mbili na AZ Alkmaar.
PSV Eindhoven v AC Milan
-AC
Milan waliitoa kwa Bao za Ugenini PSV walipotoka Sare ya Jumla ya Bao
3-3 katika Nusu Fainali za Msimu wa 2004/05. Kikosi cha Carlo Ancelotti
kilishinda Mechi ya kwanza 2-0 kwa Bao za Andriy Shevchenko na Jon Dahl
Tomasson. Katika Mechi ya Marudiano, Park Ji-Sung– ambae sasa amerudi
PSV kwa Mkopo – na Phillip Cocu walifunga Bao kwa PSV lakini Massimo
Ambrosin akaipigia Bao la 3 AC Milan kwenye Dakika za Majeruhi na Cocu
kuifungia PSV na Mechi kuwa 3-3.
-Kwa sasa Kocha wa PSV ni Cocu ambae pia
alicheza Mechi kati ya Timu hizi Msimu wa 2005/06 ambapo walitoka 0-0
na PSV kushinda 1-0 kwenye Marudiano wakiwa Nyumbani huku Bao la ushindi
likifungwa na Jefferson Farfán (Dakika ya 84) huku Beki wa AC Milan,
ambae aliwahi kuwa Beki wa PSV na Man United, Jaap Stam akitolewa nje
kwa Kadi Nyekundu.
FC Viktoria Plzeň v NK Maribor
-Plzeň
wameshinda Mechi zao zote 10 za Raundi za Mchujo za UEFA CHAMPIONZ LIGI
za Msimu wa 2011/12 na Msimu huu wakifunga Jumla ya Bao 34.
-Kwa Maribor hii ni mara ya 11 wanacheza
UEFA CHAMPIONZ LIGI lakini ni mara moja tu, Msimu wa 1999/2000, ndio
wameweza kufika hatua ya Makundi.
JUMATANO
GNK Dinamo Zagreb v FK Austria Wien
-Rekodi ya Nyumbani ya hivi karibuni ya Dinamo ni nzuri kwani wameshinda mara 8 mfululizo.
-Mara pekee kwa FK Austria Wien kucheza na Klabu ya Croatia ni Sare ya 2-2 na
HNK Hajduk Split Msimu wa 1977/78 kwenye Robo Fainali ya European Cup Winners ambayo walishinda kwa Penati.
PFC Ludogorets Razgrad v FC Basel 1893
-Mara
pekee ambayo PFC Ludogorets Razgrad imecheza Ulaya ni Msimu uliopita
ilipotolewa na GNK Dinamo Zagreb katika Raundi ya Pili ya Mchujo ya
Mashindano haya.
-Mara pekee kwa FC Basel kucheza na
Klabu kutoka Bulgaria ni kwenye Makundi ya EUROPA LIGI Msimu wa 2009/10
walipoitoa PFC CSKA Sofia BAO 2-0 Ugenini na 3-1 Nyumbani.
FC Steaua Bucureşti v Legia Warszawa
-Mara pekee kwa Steaua kucheza na Klabu ya Poland ni Msimu wa 2007/08 kwenye Mashindano haya ambapo waliitoa Zagłębie Lubin.
-Tangu Msimu wa 1995/6 washiriki hatua
ya Makundi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI, Legia Warszawa hawajafika tena huko
na mara mbili walikaribia walipotolewa Raundi ya Mchujo ya mwisho na FC
Barcelona Mwaka 2002/03 na FC Shakhtar Donetsk Mwaka 2006/07.
FC Schalke 04 v PAOK FC
-Kocha
mpya PAOK, Huub Stevens, amepata umaarufu akiwa na Schalke, ambako
Mwaka 1997 alitwaa UEFA Cup na pia German Cup Miaka ya 2001 na 2002.
Fenerbahçe SK v Arsenal FC
-Mara
ya mwisho kwa Arsenal kutembelea Sükrü Saraçoglu Stadium walishinda Bao
5-2 kwenye Mechi ya Makundi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI Msimu wa 2008/09
walipoirarua Fenerbahçe na kumaliza Rekodi yao ya kutofungwa Mechi 15 za
Nyumbani za Mashindano ya Ulaya.
-Wachezaji wa sasa wa Fenerbahce ambao
wamewahi kucheza England ni Emre Belözoğlu (Newcastle United FC
2005–08), Dirk Kuyt (Liverpool FC 2006–12), Raul Meireles (Liverpool FC
2010–11 na Chelsea FC 2011–12) pamoja na Joseph Yobo (Everton FC
2002–10).
EUROPA LIGI
RATIBA:
Alhamisi Agosti 22
Kuban Krasnodar v Feyenoord
Zulte Waregem v Apoel Nicosia
Rapid Vienna v Dila Gori
Pandurii Targu-Jiu v Braga
Tromso v Besiktas
Apollon Limassol v Nice
Aktobe v Dynamo Kiev
Swansea v Petrolul Ploiesti
Atromitos v AZ
FH Hafnarfjordur v Genk
IF Elfsborg v FC Nordsjaelland
Slask Wroclaw v Sevilla
SV Red Bull Salzburg v VMFD Zalgiris
FK Karabakh v Eintracht Frankfurt
Minsk v Standard Liege
Jablonec v Real Betis
Rijeka v VfB Stuttgart
Chornomorets v Skenderbeu
Maccabi Tel-Aviv v PAOK Salonika
St Gallen v Spartak Moscow
Molde v Rubin Kazan
Vojvodina v FC Sheriff
Trabzonspor v FK Kukesi
Esbjerg v Saint Etienne
Grasshoppers v Fiorentina
Maccabi Haifa v FC Astra Giurgiu
Udinese v Slovan Liberec
Dinamo Tbilisi v Spurs
Estoril Praia v FC Pasching
Nomme Kalju v Dnipro
Partizan Belgrade v FC Thun
*** Marudiano ni Agosti 29.
The superonenews.blogspot.com
0 comments:
Post a Comment