Tuesday, August 20, 2013

LIGI KUU ENGLAND: MAN CITY WAFANYA MAUAJI!!!! MANCHESTER UNITED v CHELSEA KUCHEZA JUMATATU USIKU


PELLEGRINI-KIDOLE
BOSI mpya wa Manchester City Manuel Pellegrini Usiku huu ameanza himaya yake kwa ushindi mnono baada ya Kikosi chake kuichapa Newcastle Bao 4-0 katika Mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu England kwa Msimu wa 2013/14 iliyochezwa Uwanja wa Etihad.


BPL2013LOGO
MAGOLI:
-Silva 6
-Aguero 22
-Toure 50-Nasri 75

KABLA ya Mechi hii kuanza, Man City walimuenzi Kipa wao wa zamani Marehemu Bert Trautmann ambae aliwahi kuwa Kocha wa Tanzania aliefariki Dunia Tarehe 19 Julai 2013 huko Spain kwa kuvaa Jezi maalum za Kijani zenye Nambari 1 mgongoni wakati wakipasha moto na pia Timu zote mbili na Watu wote Uwanjani walisimama wakishangilia kwa Dakika Moja ikiwa ni heshima kwake.
Trautmann alikuwa Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania kati ya Miaka ya 1975 na 1978.
Katika Mechi hii, Newcastle walilazimika kucheza Kipindi chote cha Pili wakiwa Mtu 10 baada ya Beki wao Steven Taylor kupewa Kadi Nyekundu kwa kumpiga kiwiko Sergio Aguero katika Dakika ya 47.
VIKOSI:
Man City: Hart, Zabaleta, Kompany, Lescott, Clichy, Fernandinho, Toure, Jesus Navas, Aguero, Silva, Dzeko
Akiba: Milner, Nasri, Negredo, Kolarov, Javi Garcia, Rodwell, Pantilimon.
Newcastle: Krul, Debuchy, Coloccini, Steven Taylor, Yanga-Mbiwa, Sissoko, Tiote, Gouffran, Ben Arfa, Gutierrez, Cisse
Akiba: Anita, Elliot, Marveaux, Shola Ameobi, Obertan, Sammy Ameobi, Dummett.
Refa: Andre Marriner
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA
[SAA NI ZA BONGO]
Jumatano Agosti 21
21:45 Chelsea v Aston Villa
Jumamosi 24 Agosti
14:45 Fulham v Arsenal
17:00 Everton v West Bromwich Albion
17:00 Hull City v Norwich City
17:00 Newcastle United vWest Ham United
17:00 Southampton v Sunderland
17:00 Stoke City v Crystal Palace
19:30 Aston Villa v Liverpool
Jumapili 25 Agosti
18:00 Cardiff City v Manchester City
18:00 Tottenham Hotspur v Swansea City
Jumatatu 26 Agosti
22:00 Manchester United v Chelsea

0 comments:

Post a Comment