Friday, July 26, 2013

ZIARA JAPAN: MAN UNITED APONEA CHUPUCHUPU,,ARSENAL WANG'ARA

MAN_UNITED-CLEVERLEY_N_ZAHA
Man United leo wamemaliza Ziara yao Nchini Japan kwa kutoka Sare ya Bao 2-2 na Cerezo Osaka katika Mechi ambayo walikuwa nyuma kwa Bao 2-1 hadi Dakika ya 91 na ndipo Mchezaji mpya Wilfried Zaha alipofunga Bao la kusawazisha likiwa Bao lake la kwanza kwa Timu yake.
Awali, ‘Mtoto wa Nyumbani’, Shinji Kagawa, akicheza dhidi ya Timu yake ya zamani, alikosa Penati iliyozuiwa na Kipa Jin Hyeon na kuwa Kona ambayo ilizaa Goli la Man United ambalo alifunga Kagawa na kuamsha nderemo Uwanja mzima.
MAGOLI:
Cerezo Osaka 2
-Sugimoto 34
-Minamino 63
Man United 2
-Kagawa Dakika ya 54
-Zaha 91
Man United wanaelekea huko Hong Kong kucheza Mechi yao ya mwisho Bara la Asia hapo Jumatatu Julai 29 dhidi ya Kitchee Uwanja wa Hong Kong.
VIKOSI:
CEREZO OSAKA: Jin Hyeon, Sakemoto, Fujimoto, Yama, Maruhashi, Yokoyama, Kusukami, Fabio, Sugimoto, Minamino, Edno
Akiba: Takeda, Tada, Moniwa, Araiba, Bando, Yoshino, Edamura, Kurogi, Akiyama, Kogure, Mukuhara
MAN UNITED: Lindegaard; Rafael (Fabio 79), Smalling, Ferdinand, Buttner (Evra 79); Young (Cleverley 79), Giggs (Lingard 79), Jones (Anderson 46), Kagawa  (Zaha 58), Welbeck, Van Persie (Januzaj 69)
Akiba hawakutumiwa: De Gea, Amos, Keane
MANCHESTER UNITED==ZIARA:
Julai 13 Singha All Star 1 Man United 0
Julai 20 A-League All Stars 1 Man United 5
Julai 23 Yokohama F-Marinos 3 Man United 2
Julai 26 Cerezo Osaka 2 Man United 2
Julai 29 Kitchee (Hong Kong Stadium, Hong Kong) [Saa 9 Mchana]
Agosti 6 AIK Fotboll (Friends Arena, Stockholm)
Agosti 9 Sevilla (Old Trafford - Rio Ferdinand Testimonial) [Saa 3.30 Usiku]
URAWA REDS 1 ARSENAL 2
Wakicheza Mechi yao ya 4 huko Asia, Arsenal leo wameendeleza wimbi lao la ushindi kwa kuifunga Urawa Reds Bao 2-1 katika Mechi iliyochezwa Saitama Stadium, Saitama.
MAGOLI:
Urawa Reds 1
-Abe Dakika ya 58
Arsenal 1
-Podolski Dakika ya 48
-Apkom 82
Arsenal wamemaliza Ziara yao huko Bara la Asia na sasa wanarudi London ambako Agosti 3 na 4 Uwanjani kwao Emirates watacheza Mashindano yao wenyewe kugombea Emirates Cup kwa Mechi na Napoli na Galatasaray.
VIKOSI:
ARSENAL: Fabianski; Sagna Koscielny, Mertesacker (Jenkinson 46), Miquel; Arteta (Rosicky 46) Wilshere (Ramsey 46) Oxlade-Chamberlain; Walcott, Gnabry (Miyaichi 46); Giroud (Podolski 46)
Akiba hawakutumiwa: Szczesny, Martinez, Gibbs, Olsson, Aneke, Eisfeld, Zelalem, Akpom
URAWA REDS: Yamagishi; Tsuboi, Nasu, Abe, Ugajin; Kojima, Kashiwagi, Umesaki, Richardes; Yamada, Koroki
Akiba hawakutumiwa: Kato, Otani, Yamada, Nagata, Nagata, Okamoto, Hirakawa, Nozaki, Yajima, Sekiguchi, Sakano
ARSENAL-ZIARA:
Julai 14 Indonesia XI (Gelora Bung Karno Stadium, Jakarta) =USHINDI 7-0
Julai 17 Vietnam (My Dinh National Stadium, Vietnam) =USHINDI 7-1
Julai 22 Nagoya Grampus (Toyota Stadium, Japan) =USHINDI 3-1
Julai 26 Urawa Red Diamonds (Saitama Stadium, Japan) =USHINDI 2-1
Agosti 3 Napoli (Emirates Cup) SAA 12.20 JIONI
Agosti 4 Galatasaray (Emirates Cup) SAA 12.20 JIONI
Agosti 10 Manchester City (Olympic Stadium, Helsinki) SAA 11 JIONI

0 comments:

Post a Comment